Teknolojia ya kuwasiliana na mpenzi wako kupitia ndoto

Teknolojia ni Yetu sote

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2020
Posts
620
Reaction score
1,240

Hivi unajua unaweza kuwasiliana na mpenzi wako kupitia ndoto yani mmelala wawili lakini inawapa nguvu ya kufanya mazungumzo kwa njia ya ndoto kupitia usingizi.

Wana sayansi kutoka marekani kwenye Jiji la California wamefanikiwa kutengeneza kifaa kinaitwa Remspace kinachosaidia watu wawili wakiwa wamelala kuweza kufanya mawasiliano kupitia ndoto nzuri.


Kifaa icho cha Remspace (Rapid eye movement) ambapo unakivaa kama miwani mtu mmoja atakayewahi kupata usingizi na kuanza kuota basi kifaa icho kinawasiliana na ubongo 🧠 Kisha kinachukua taswira ya picha na kuhamisha kwa mwenzako.


Taarifa izo zina safarishwa kupitia mfumo mkuu ambao ulikua unafuatilia ndoto Kisha unawasiliana na ubongo kupitia maneno tofauti tofauti ambayo tunaweza kuita ni lugha ya Remmyo. Inatengeneza neno linaitwa zhilak kupitia earbuds ulizovaa Kisha kuanza kuwasiliana kwenye ndoto.

Mwanzilishi wa Remspace CEO Mr Michael Raduga alisema " miaka ya nyuma kuwasiliana kwenye ndoto ilikua inaonekana kama ni kama vile hadithi ya kisayansi lakini Amini kesho itakua kitu cha kawaida hatutaweza kufikiria maisha Yetu bila teknolojia hii."
 

Attachments

  • a-new-dimension-a-dream-a-nightmare-ambient-dark-night-v0-exzkwvcpss7c1.png
    231.7 KB · Views: 7
Vipi kwa watu wenye insomnia, sleeping disorder ambak ku achieve REM sleep ni changamoto wao si watakuwa kama wamewatenga😁😁😁
 
Kwanini msipumzike mkawasiliana kesho kwa mdomo?ndio maana watu wanakufa kwa stress,kuchosha ubongo tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…