Ray J Enterprise
Member
- Jul 18, 2022
- 49
- 57
MATUMIZI YA MITA KWENYE MITUNGI YA GESI
Utangulizi
Tanzania ni miongoni mwa nchi zenye hifadhi kubwa ya gesi asilia. Ripoti mbalimbali zinaonyesha kwamba Tanzania inakadiriwa kuwa na gesi asilia yenye ujazo wa mita trilioni 230, ingawa imethibitishwa hadi sasa ni futi trilioni 57.54. Kutokana na wingi wa gesi asilia, nchi ya Tanzania inashika nafasi ya 82 duniani. Tayari maeneo mbalimbali nchini Tanzania yameanza kuchimba gesi asilia kama vile visiwa vya Songosongo-Kilwa na eneo la Msimbati mkoani Mtwara.
Pamoja na wingi wa hifadhi ya gesi asilia, Tanzania bado inategemea mafuta kuendesha mitambo ya viwanda, magari na jenereta kuzalisha umeme. Lakini pia hutegemea nishati ya kuni na mkaa kwa upande wa nishati ya kupikia majumbani. Kwa sasa, kumekuwa na shinikizo kubwa duniani la matumizi ya gesi asilia katika shughuli za kila siku ikiwa ni sehemu ya kampeni ya kuokoa mazingira. Gesi asilia imeanza kutumika katika shughuli za nyumbani kama nishati mbadala ya kupikia.
Itakumbukwa kuwa asilimia kubwa ya Watanzania wanatumia nishati ya kuni na mkaa kwa wingi kuliko nishati ya gesi ambayo ni rafiki wa mazingira kwa sababu inatoa kiasi kidogo cha hewa ukaa. Kwa mujibu wa ripoti mbalimbali za hali ya upatikanaji wa nishati zinazotolewa na ofisi ya taifa ya takwimu na wakala wa nishati vijijini (REA) zinaonyesha kwamba kaya za Tanzania bara zinazotumia gesi asilia majumbani kwa ajili ya kupikia ni chini ya asilimia tatu. Kwa mwaka 2020 watumiaji wa nishati ya gesi majumbani ilikuwa ni asilimia 1.5 ya kaya zoteTanzania bara.
Kwa nyakati tofauti serikali imeendelea na jitihada za kusitisha matumizi ya mkaa na kuni nchini Tanzania kwa sababu nishati hizo si salama kwa afya za walaji na mazingira kwa ujumla. Taarifa ya hali ya mazingira nchini Tanzania kwa mwaka 2019 inaonesha kuwa kasi ya uharibifu wa misitu ni kubwa na kila mwaka zaidi ya hekta 469,420 huharibiwa kutokana na ukataji wa miti kwa ajili ya matumizi ya kuni na mkaa. Kutokana na athari hizo za mazingira zinazosababishwa na ukataji miti kwa ajili ya kuni na mkaa, serikali kupitia ofisi ya makamu wa rais imezitaka taasisi zote za umma na binafsi nchini Tanzania kuacha matumizi ya kuni na mkaa ifikapo mwaka 2024.
Tamko hili ni utekelezaji wa dira ya taifa ya matumizi ya nishati safi ya kupikia pamoja na mpango mkakati wa utekelezaji wa dira kwa kipindi cha miaka 10 hadi 2033. Kwa maneno mengine tunaweza kusema kwamba dira hii na mkakati huu kwa pamoja unahimiza matumizi ya gesi asilia ambayo ni rafiki kwa mazingira badala ya kutumia kuni na mkaa ambao umekuwa kichocheo kikubwa cha uharibifu wa mazingira. Kwa jitihada hizi za serikali na wadau binafsi wa mazingira, ningependa kuona baadhi ya changamoto za matumizi ya gesi ya majumbani zikitatuliwa. Imekuwa ni kero sana wakati mwingine tunanunua mitungi ya gesi ikiwa haijajazwa vizuri na hata gesi ikiisha hujui ni kiasi gani cha gesi ndani yake au kilichobaki. Katika ulimwengu wa sasa wa sayansi na teknolojia ni jambo ambalo halikubaliki.
MATUMIZI YA MITA KWENYE MITUNGI YA GESI
Teknolojia hii itasaidia mtumiaji wa gesi kutambua kiasi cha gesi wakati wa ununuzi na wakati wa matumizi. Mtumiaji atajua asilimia zinazoonyesha kiwango cha gesi kama ilivyo katika asilimia ya chaji ya betri kwenye simu au kiwango cha salio la umeme kupitia mita za umeme. Wakati mwingine wateja wanaibiwa sana kwa kutouziwa gesi yenye ujazo kamili kutokana na kutojua kiasi kilichomo katika mtungi wa gesi.
Teknolojia hii itasaidia kuondoa changamoto hii na kuongeza uwajibikaji kwa makampuni yanayojihusisha na uuzaji wa gesi asilia kuuza gesi yenye ujazo kamili na hivyo kurahisisha wakala wa vipimo nchini pamoja na tume ya ushindani FCC kutokana na malalamiko ya wateja. Pia teknolojia hii itamsaidia mteja kutumia gesi yake vyema kutokana na kipato chake badala ya kutojua kiasi cha gesi iliyomo.
Kwa maana hii, teknolojia hii itapunguza migogoro ya kisaikolojia na kifamilia, hasa kipindi ambacho gesi inaisha na hakuna fedha za kujaza gesi. Hivyo mtumiaji atatumia gesi kulingana na hali ya kipato chake huku akijua kiasi kinachotumika wakati wa kupikia. Sote tunajua namna ambavyo TANESCO walikuja na mtindo wa namna hii kumuwezesha kujua kiasi cha umeme kilichopo na kilichotumika yaani Lipia Umeme Kadri Unavyotumia (LUKU). Kadhalika, mfumo huu utatumika kwenye gesi majumbani na kwa vyovyote vile kampuni itakayosambaza gesi yake kwa mfumo huu itapata wateja wengi kwa kuwa teknolojia hii ni muhimu sana kwa watumiaji wa gesi nchini Tanzania.
HITIMISHO
Ili kutekeleza dira ya taifa ya matumizi ya nishati safi kwa kupikia pamoja na mpango mkakati wa utekelezaji wa dira ni vyema utekelezaji huu ukaenda sambamba na matumizi ya teknolojia mbalimbali ili kukidhi kiu na mahitaji ya mtumiaji wa mwisho, ikiwa ni pamoja na matumizi ya mita katika kulinda matumizi ya gesi majumbani. Halikadhalika, sera na mkakati huu lazima viweze kutatua changomoto zote zinazojitokeza katika maisha ya kila siku ya mtumiaji wa mwisho ili kufikia malengo ya maendeleo endelevu hususani lengo namba 7 ambalo linasisitiza sana upatikanaji wa nishati ya kisasa kwa gharama nafuu kwa watu wote duniani. Kwa maana hiyo basi changomoto hii ya kukosekana mita ya kusoma kiwango cha gesi katika mitungi ya gesi majumbani inapaswa kuwa sehemu ya suluhisho la haraka la sera na mkakati huu wa matumizi ya nishati safi ili kunusuru uharibifu wa mazingira na upatikanaji wa nishati bila vikwazo.
Ikiwa utavutiwa na andiko hili basi nakuomba sana kwa unyenyekevu unipigie kura kwa kubonyeza neno vote. Asanteni sana!

Upvote
5