Teknolojia ya Vijidudu Vidogo Vidogo (Effective Microorganisms) Kwenye Kilimo, Ufugaji na Samaki

Teknolojia ya Vijidudu Vidogo Vidogo (Effective Microorganisms) Kwenye Kilimo, Ufugaji na Samaki

Tango

Member
Joined
Mar 13, 2008
Posts
58
Reaction score
5
Utangulizi

EM.1®️ ni teknolojia
iliyogunduliwa nchini Japan miaka ya 80. Imesajiliwa Tanzania na Kampuni ya Feedpro EMAx Limited mwaka 2018. EM ni kifupisho cha Effective microorganisms ambao ni mfumo wa vijidudu hai, salama kwa binadamu. Hii teknolojia inatumika kwenye nchi zaidi ya 110 duniani na pia inazalishwa kwenye nchi zaidi ya 70 duniani. EM.1®️ kwa Tanzania imesajiliwa kutumika kwenye kilimo, ufugaji, uboreshaji wa mazingira na gesi ya kibaolojia (biogas).

Matumizi ya EM.1®️ kwenye Kilimo: Teknolojia ya EM.1®️ inaweza kutumika kutengeneza mboji. Inawezesha mbolea ya wanyama kuoza kwa haraka kwa kuifanya ichachuke na hivyo kufanya wadudu ambao wanatokea kwenye mbolea watokee haraka. Uwepo wa wadudu kwenye ardhi unasaidia kuboresha ubora wa ardhi na hivyo kufanya mimea kupata virutubisho vinavyostahili. Inaweza kutumika kama kifukuza wadudu na pia kama booster. Kiwango cha EM kinachotumika ni kidogo sana. EM inaleta tija kwenye uzalishaji wa mara mbili zaidi na kuokoa gharama kwa zaidi ya asilimia 70.

Matumizi EM.1®️ kwenye Mifugo: EM.1®️ inatumika kwenye mifugo kwa kuchanganya kwenye maji ya kunywa ama kwenye chakula cha wanyama, kuwaongezea hamu ya kula pia. Inaondoa harufu mbaya kwenye mabanda hasa kwa wafugaji wa mjini. EM.1®️ inasaidia kuongeza mmeng’enyo wa chakula na hivyo kuwepo na uchukuaji wa chakula kingi zaidi mwilini mwa mnyama. EM.1®️ imethibitika kuongeza ubora wa nyama, mayai, maziwa na ukuaji wa wanyama wa kufugwa.

Matumizi ya EM.1®️ kwenye Mazingira: EM.1®️ inatumika kuchakata taka za majumbani kwa kutengeneza mbolea ama wadudu ambao wanaweza kutumika kulishia kuku. Taka za jikoni zinaweza kukaa hadi miezi mitano kwenye pipa bila kutoa harufu wala kujaa kwani wadudu wanaozalishwa baada ya kuvundikwa na vijidudu vya EM.1®️ hula masalia na mabaki ya chakula. Inatumika kushusha ujazo wa vyoo vya shimo kwa wastani wa kipenyo cha mita moja kwa hasi ½ mita kwa wiki 3 tu. Inatumia pia kuondoa harufu mbaya kwenye vyoo, masoko, sehemu za umma, machinjio, na kadhalika.

Bidhaa za EM: Bidhaa mama inaitwa EM.1®️ ambayo lita moja ikichanganywa na molasis lita moja na lita 18 za maji unapata lita 20 za EM iliyoendelezwa kwa muda wa siku 7. Lita 20 za EM iliyoendelezwa zinazotokana na lita moja ya EM.1®️ inaweza kutumika kwa hadi lita 10,000 za maji ya kumwagilia au ya kunywa wanyama. Inaweza kutumika kwenye mbolea ya hadi tani 8. Na pia inaweza kutumika kutengenezea mboji ya hadi tani 4.

Pakua Mwongozo wa Matumizi ya EM.
 

Attachments

  • MWONGOZO TEKNOLOJIA YA EM TANZANIA final PRINT_WEB.pdf
    MWONGOZO TEKNOLOJIA YA EM TANZANIA final PRINT_WEB.pdf
    1.5 MB · Views: 22
  • Vijidudu EM.jpeg
    Vijidudu EM.jpeg
    27.8 KB · Views: 4
  • Vijidudu EM2.jpeg
    Vijidudu EM2.jpeg
    150.6 KB · Views: 5
Back
Top Bottom