Televisheni za kitaifa UTV, ITV, CH10 na TBC1 mnaharibu Lugha (mnawachanganya wananchi)

N'yadikwa

JF-Expert Member
Joined
Aug 10, 2014
Posts
7,427
Reaction score
10,905
TBC1 na ITV - Ninyi mnatofautiana kuandika neno MBASHARA? MUBASHARA?

USHAURI: Nendeni BAKITA wawapatie neno sahihi maana inaonekana mnashindana wananchi hatuelewi LIPI ni neno sahihi? MUBASHARA? au MBASHARA?!!

Mnaipotosha jamii ambayo hujifunza lugha kupitia kwenu.

CHANNEL 10 na UTV

Kwanini mtumie neno LIVE ambalo si la kiswahili? Tumieni kiswahili ama laah tuelewe matangazo yenu yanarushwa kwa lugha ya kiingereza.

Msichanganye lugha hata kanuni za Utangazaji zinakataza ninyi mnakiuka makusudi?

REJEENI PICHA HAPO CHINI View attachment 1647204View attachment 1647205View attachment 1647206

 
Watayarishaji wao hawana weledi kwa kifupi, hawajuwi kazi zao.
 
UTV, ITV na channel 10 ni televisheni za Taifa kumbe
 
Ndio kawaida yao!mdada,mkaka,takikana mashule,taradadi
 
Neno "mubashara" (herufi 9)ni refu mno. Ndio sababu wengine wanaona bora waseme "Live" (herufi 4). Nashauri litumike neno "Mub." au "Muba." kama kifupi cha mubashara.
 
Neno "mubashara" (herufi 9)ni refu mno. Ndio sababu wengine wanaona bora waseme "Live" (herufi 4). Nashauri litumike neno "Mub." au "Muba." kama kifupi cha mubashara.
[emoji1] hiyo kali mwanabodi!!

Sent from my SM-A705FN using JamiiForums mobile app
 
Reactions: SMU
مباشر

Mubashir (Kiarabu)

Waswahili tukaita mubashara.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…