Telexfree - Does not Make Economic Sense;

Logikos

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2014
Posts
15,460
Reaction score
24,233
Wakuu baada ya kuzidi kusumbuliwa na ndugu zetu kujiunga kwenye hii kitu na watu kukataa kabisa kwamba hii sio Ponzi Scheme naomba hao watu watueleze hizo pesa zinatoka wapi...

Products
Kwakweli hio product yao VOIP haina uzuri wowote na katika karne hii ya free internet communications products kama Skype; Whatsapp n.k. hii yao ni ya gharama amabayo hata bure mtu asingetumia.. (kwahio haiuziki na kuna better alternatives)

Matangazo
Hivi ni kampuni gani itakulipa pesa zote hizo kwa ku-post matangazo kwa siku ? tena kwenye free sites ?, Ku-post matangazo kungekuwa kunalipa hivyo mimi ningeomba watu waniajiri niwe ninapost matangazo kila siku na kila dakika, na hapa swali ni kwamba unalipwa commission sababu ya kutuma matangazo au unalipwa commission sababu ya pesa unazotoa ili utume matangazo ?

Hitimisho

Jamani tuwe wa kweli tu na kama mtu unajiunga hapa fahamu kabisa kwamba unajiunga ili kuwatapeli watu pesa zao, wengi wanapata na wengi wataendelea kupata ila fahamu kwamba mwisho wa siku hicho unachopata wewe kitawaumiza wengine, pia hii ni kama Kamali siku yoyote likifumuka fahamu kwamba pesa yako itapotelea huko

Kwa maelezo zaidi ya hii kampuni unavyoweza kupata (kupoteza) pesa
TelexFree Review: Spam the internet for $20 a week | BehindMLM
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…