Temba apandishwa mahakamani kwa kutishia kuua

brave one

JF-Expert Member
Joined
Feb 5, 2013
Posts
4,879
Reaction score
7,386
Msanii kutoka TMK Wanaume Family, Amani James aka Mh Temba jana amefikishwa katika mahakama ya mwanzo ya Temeke jijini Dar es salaam akikabiliwa na mashitaka ya kutishia kuua kwa kisu kutokana na wivu wa mapenzi.

Kwa mujibu wa Nipashe, Temba alipandishwa kizimbani na kusomewa mashitaka yake mbele ya hakimu Claudia Frank wa mahakama hiyo.

Mheshimiwa Temba alifikishwa mahakani hapo mapema saa 3:00 asubuhi huku akiwa amefungwa pingu chi ya ulinzi wa askari kanzu wa kituo cha Mkoa wa Kipolisi Chang'ombe. Aliwekwa chini ya ulinzi katika kituo cha mahabusu ya mahakama hiyo kabla ya kusomewa mashitaka yake. Kesi hiyo imesajiliwa mahakamani hapo kwa namba 371 chini ya kifungu cha 89 kidogo cha (2) (a) sura ya 16 ya mwenendo wa sheria ya Makosa ya Jinai.

Akisomewa mashitaka na karani wa mahakama hiyo, Joyce Ngamesha, alidaiwa kuwa Januari 28, mwaka huu, saa 1:00 jioni katika baa ya Scorpion Iiliyopo Temeke jijini Dae es salaam, mshitakiwa alimtishia
kumchoma kisu Godrey Deogratius ama Sulla.

Mshitakiwa alikana mashitaka hayo na yupo nje kwa dhamana. Hakimu Frank alisema kesi hiyo itasikiliza ushahidi March 11, mwaka huu. Kabla ya kufikishwa mahakamani hapo, Mshitakiwa alifikishwa katika kituo cha polisi cha Chang'ombe akituhumiwa kutishia kumchoma kisu mlalamikaji kwa madai ya kuwa na mahusiano wa kimapenzi na mke wa msanii huyo.

Ilidaiwa kuwa mshitakiwa alimtishia kumchoma kisu mlalamikaji huku akijua ni kinyume na sheria.


Source: Nipashe
 
Kama wivu ulikuwa ni kwa Mke wake amechelewa sana angeuwa!
 
Sasa anatoka puvu la nini? Huyo mke wake mwenyewe ndio aseme nae...ngoja afungwe halafu watu wawe wanapiga ndani kwake ndio apate akili.
 
Temba nae..kumegewa no siri ya ndani,sasa yeye kaleta hasira matokeo yake mpaka jamuhuri imejua sasa kua jamaa kamegewa!
 
next thing ana-release album...they call it showbiz.
 
"Muda ulipofika umeme si ukakatikaaaa/
Utadhani Tanesco walijua kwamba leo mi ntaua/ Umekuja kuwaka tumechoka nyakanyaka....."


Ndo huyu demu aliyemegewa?
 
Dah... Kumegewa siri ya ndani jama.!

Afungwe tu. Tumechoka.
 
"Muda ulipofika umeme si ukakatikaaaa/
Utadhani Tanesco walijua kwamba leo mi ntaua/ Umekuja kuwaka tumechoka nyakanyaka....."


Ndo huyu demu aliyemegewa?
kama unamsema huyo anaetokea kwenye hiyo video ameshafariki
 
Yupo gpsa pale kurasini huyo mdada ni mweupe tu madereva wa serikali wanajipigia tu wala siyo mchoyo sijui atawachoma wangapi hvyo visu
Watu wanasubiri afungwe tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…