Hii kitu inawezekana kabisa. Ndiyo maana Pape kasema tembea uone. Huwezi kusema hiyo ni photoshop kama tu hujatembea dunia yote ukawaona watu wa aina tofautitofauti. Binadamu tunatofautiana kwa kiasi kikubwa sana huwezi kuamini. Kuna wakati nilikwenda Bukoba nikamkuta mmama ana makalio ambayo kwa namna yoyote ile unaweza kuona kwamba siyo ya kawaida. Kwa sababu ni makubwa sijawahi yaona pengine na sitegemei kuyaona tena. Kama mtu angepiga picha yale akayaleta hapa wote tungejua ni photoshop. Lakini ni ukweli huo kwamba binadamu tunatofautiana sana.