Tembo akisifiwa sana tutaendelea kuumia

Tembo akisifiwa sana tutaendelea kuumia

muzi

JF-Expert Member
Joined
Jun 17, 2016
Posts
1,041
Reaction score
1,457
Tanzania nafikiri kuna sehemu tunakosea sana, kuna watu wanasifiwa mpaka tunakufuru kwa maneno yetu. Hatukatai kumsifia mtu akifanya mazuri lakini iwe na kiasi.

Sifa, heshima, utukufu, na tukufu zote ziende kwa mwenye kutoa uzima, uhai, ambaye ni Muumba wa mbingu na nchi. Sasa inashangaza mtu mmoja ndiye anafanyiwa hayo tena kama vile pesa anatoa kwenye mfuko wake. Hapana, hapana.

Ila kama tukiendelea kumtukuza binadamu tutaendelea kupigwa na majanga maana inakuwa tumegeuza binadamu kama ndiye Mungu wetu, yetu macho tuendelee na siasa za maji taka za kusifia binadamu kupitiliza kuliko Muumba wa mbigu na nchi.

Nisiseme mengi maana inatia hasira
 
Dah. Umetuacha mbali kidogo. Fafanua
 
Tumezindua Mbezi stand na ubungo flyover..next step dar yote tunaipiga chini
 
Kabudi alisema Mheshimiwa Mungu! akimaanisha Mh. Magufuli
 
Ukishajua anachopenda bosi wako lazima kila staff atafanya hata maigizo/hila kusema au kufanya yale unayotaka yeye
Hii yote ugali upatikane na maisha yaende mbele, hii ndo shida kubwa ya umasikini wa fikra na kuweka maisha yako kuwa tegemezi kwa binadamu mwenzako
Pamoja na yote kila chenye mwano hakikosi kuwa na mwisho
 
Washajua anachopenda mzee?
 
Mshahara wa dhambi ni mauti bali karama ya Mungu ni uzima wa milele
 
Ukishaona unakutana na mapigo ya magonjwa, njaa, dhiki, misiba, kiangazi n.k ni WAKATI WA KUMRUDIA MUNGU NA KUOMBA TOBA/MSAMAHA WA KWELI
 
Wamtumainio BWANA ni kama mlima Sayuni, Ambao hautatikisika, wakaa milele.
 
Back
Top Bottom