DOKEZO Tembo waendelea kuwataabisha wanakijiji wa Mgagao wilayani Mwanga, Kilimanjaro, hazina msaada wowote

DOKEZO Tembo waendelea kuwataabisha wanakijiji wa Mgagao wilayani Mwanga, Kilimanjaro, hazina msaada wowote

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Tunzo

JF-Expert Member
Joined
Feb 1, 2013
Posts
4,082
Reaction score
2,402
Makundi ya tembo yanataabisha wanakijiji hawa, ni hatari kubwa, hakuna kulala, ni kukesha, na mchana yapo, hata mda huu wa saa nne usiku nasikia mavuvuzela na kupiga madebe kuyasogeza

Maafisa wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) wanafika wanakuja na kuondoka hawana msaada, wowote, naona sasa hivi wamebaki wenyewe tu kupambana nayo,

Utalii wa ndani umehamia kijiji hiki, kama hujaona tembo sogea hapa utawashuhudia.
 
Watoeni pembe hizi ni dili hapa Duniani
 
Tembo wamekuwa wengi sana nchi hii kiasi cha kuingia kwenye makazi ya wananchi. Hii ni dalili nzuri na ni ishara kuwa ujangili umeisha. Ila tembo aisee ni wababe, wanaingia vijijini mchana kweupe, wanakula mazao ya wakulima kibabe hata kama yapo juu ya tembe na darini. Wanakula hadi matikikiti, mapapai, mihogo, miwa na chochote wanachoona ni chakula kitamu kwao. Kuna kampeni za serikali zinawataka wananchi kuwaepuka tembo na wanyama wengine wakali kutowakaribia zinazoendeshwa na mamlaka ya uhifidhi wanyamapori nchini TAWA. Wapo wanyama wengine wanaoingia kwenye makazi ya wananchi wakitafuta vyakula vyao na maji kama simba, chui, fisi, mbweha, nyani na jamii zake na wengine wengi wadogo kwa wakubwa, ukiwaua bila ruhusa ya mamlaka ya wanyama pori sheria kali itachukua mkondo wake. Mwananchi haruhusiwi kuua wanyama hao badala yake anapewa mbinu za kuwafukuza bila kuwadhuru na yeye kudhuriwa na wanyama hao
 
Kwa wingi wa tembo walivyoongezeka bila kuvunwa au kudhibitiwa na mamlaka husika ya wanyamapori wasifike kwenye makazi ya wananchi ipo siku tembo wataingia mpaka mijini wakita mitaa ya mijini na kuleta taharuki na kizaazaa kwa wakazi wa mijini. Kuna raia hawajawahi kuwaona mubashara na hawajui tabia za tembo kiasi cha kuweza kuepukana nao wasiwaletee madhara
 
Mzigo wa jana usiku, wakiwa kwenye makazi
IMG_20230716_082722_233.jpg
 
Back
Top Bottom