Tembo wamekuwa wengi sana nchi hii kiasi cha kuingia kwenye makazi ya wananchi. Hii ni dalili nzuri na ni ishara kuwa ujangili umeisha. Ila tembo aisee ni wababe, wanaingia vijijini mchana kweupe, wanakula mazao ya wakulima kibabe hata kama yapo juu ya tembe na darini. Wanakula hadi matikikiti, mapapai, mihogo, miwa na chochote wanachoona ni chakula kitamu kwao. Kuna kampeni za serikali zinawataka wananchi kuwaepuka tembo na wanyama wengine wakali kutowakaribia zinazoendeshwa na mamlaka ya uhifidhi wanyamapori nchini TAWA. Wapo wanyama wengine wanaoingia kwenye makazi ya wananchi wakitafuta vyakula vyao na maji kama simba, chui, fisi, mbweha, nyani na jamii zake na wengine wengi wadogo kwa wakubwa, ukiwaua bila ruhusa ya mamlaka ya wanyama pori sheria kali itachukua mkondo wake. Mwananchi haruhusiwi kuua wanyama hao badala yake anapewa mbinu za kuwafukuza bila kuwadhuru na yeye kudhuriwa na wanyama hao