Eneo la Kigamboni ni moja ya sehemu ya Dar es Salaam inayokuwa kwa haraka sana. Wahamihaji ni wengi sana, wakati huo huo uboreshaji wa miundombinu ya barabara na vivuko haiendani na kasi ya ukuaji wa mji.
Kuna njia nne za kuingia na kutoka Kigamboni.
1. Kuvuka kwa pantoni Magogoni. Njia hii inatumiwa na wengi wanaokwenda mjini au kutoka kwa miguu
2. Nyerere bridge. Njia inayotumiwa na Magari, malori na daladala zinazokwenda Machinga complex
3. Njia Mpya ya Kijichi. Hutumiwa zaidi na wanaotoka Kijichi, Mbaga Kuu, n.k
4. Tuangoma/Kongowe. Njia ndefu ya mzunguko kupitia Mbagala lkn kwa wanaotoka Mkuranga na mikoa ya Kusini
Vivuko vya Magogoni vimekuwa bado ndio sehemu muhimu sana kufika katika ya jiji ila kwa miaka yote vimeshindwa kuboresha huduma zake kuwa kwenye ubora unostahili kwa wakati wote (consistency service).
Kuna wiki Huduma zinakuwa nzuri lkn kikiharibika kimoja tu hali inakuwa mbaya sana kama ilivyo sasa ambapo kimoja kimeondolewa kwenda kufanyiwa ukarabati mkubwa.
Je, hapa wataalam wetu hawakuweza kuona na kutathmini kuwa hili litatokea? Yaani engine zitafanya kazi kwa masaa kadhaa then zitahitajika kubadilishwa?
Hawakutambua chumvi inakula board yake na lazima baada ya miaka itahitajika kutengenezwa upya? Je ongezeko la watu linaendelea hawakuweza kutathmini kwamba Kivuko kikisimama kimoja tu kati ya vitatu huduma itakuwa mbovu kwa viwili vitakavyobaki?
Hivi Temesa/Wizara haiwezi kutafuta mkopo (kama mkopo ulivyoombwa na likajengwa Daraja la Tanzanite) na kununua pantoni kubwa za kisasa kutoa huduma za haraka?
Hivi pale ferry wizi wa wazi kabisa kwa wakata tiketi hauonekani? Yaani unakuja na gari jioni unapewa tiketi ya asubuhi na sababu wanayotoa eti tunachapisha nyingi ili tusipoteze muda wa madereva, ila ukifika kule chini wanasema Mashine ya ku-scan mbovu kumbe wanazikusanya na kurudisha juu zitolewe kwa magari mengine. Nashauri Serikali ijitoe, ibaki kukusanya kodi na ada nyingine stahiki!
Ushauri zaidi kwa Serikali kwa miundombinu ya barabara. Kwa kuwa kuna mkakati wa kuanzisha viwanda vipya maeneo tofauti ya Kigamboni kama kule Kisarawe Two, serikali ianze kutathmini barabara za kufika huko kwa kuwa kwa sasa kutoka kwenye round about kubwa ya kutokea Daraja la Nyerere barabara ni finyu na foleni zimeanza hasa nyakati za asubuhi na jioni, ni muhimu kuwaondoa wanaojenga kwenye maeneo ya hifadhi za barabara mapema ili yasije kutokea kama ya Kimara/Mbezi/Kibaha.
===
Pia soma: Bashungwa aagiza TEMESA kuboresha Huduma za Vivuko