TEMESA wakajifunze Mombasa kuendesha vivuko, pamoja na watu kupita bure viko imara muda wote

TEMESA wakajifunze Mombasa kuendesha vivuko, pamoja na watu kupita bure viko imara muda wote

Replica

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2017
Posts
1,681
Reaction score
8,887
Kisiwa cha Mombasa nchini Kenya kimeunganishwa na njia tatu za kuingia na kutoka kwenye mji huo mbili zikiwa madaraja ya barabara. Upande mmoja wa kuingia kisiwa humo(Likoni) ni kutumia feri kama zile zetu za Kigamboni. Sehemu hii ilishindikana kuweka daraja kutokana na kuwa njia kuu kwa meli kuingia na kutoka bandari ya Kilindini.

Watu waendeo kwa miguu hawalipi pindi wakipita kupitia pantoni. Magari, pikipiki na bajaji wakilipa tozo ili kuweza kupata gharama za uendeshaji.

Pamoja na yote hayo, feri ya Likoni inayoendeshwa na wakala wa huduma za Vivuko Kenya ina vivuko vinne. Viwili katika hivyo vikiwa na uwezo mkubwa sana huku kimojawapo kikiwa cha magari pekee.

Kwa Kigamboni pamoja na matatizo ya mara kwa mara vivuko vyetu, Temesa wameamua kumpa mtu binafsi aongeze nguvu kutokana na kushindwa kuhudumia wananchi wa Kigamboni. Wanafeli wapi! Basi wakajifunze..

AA8A1225.jpg
AA8A1212.jpg
 
Back
Top Bottom