Fakyuol
Senior Member
- Nov 26, 2023
- 148
- 325
Klabu ya Manchester United inafikiria kumpa kazi katika nafasi ya kocha mkuu, mkufunzi wa timu ya taifa ya Uingereza Gareth Southgates.
Mmiliki mwenza wa klabu hio bwana Jim Ratcliffe, anaamini kocha huyo ndie mbadala sahihi wa mwalimu wa sasa bwana Erik Ten Hag itakapo fika mwishoni mwa msimu huu. Kupitia vyanzo mbalimbali ambavyo vipo karibu na Jim Ratcliffe, vinadai kwamba mmiliki mwenza huyo ni muumini mkubwa wa mwalimu huyo raia wa Uingereza.
Mkataba wa Gareth Southgates na shirikisho la soka la Uingereza utafikia tamati mwezi December mwaka huu. Lakini licha ya juhudi mbalimbali za shirikisho hilo kumtaka asaini kandarasi mpya, mwalimu huyo ameonekana kusuasua kuongeza mkataba mpya, huku akidai atarudi kwenye meza ya mazungumzo pale tu michuano ya Euro 2024 itakapo tamatika.
#Unaambiwa