Tenda ya kusupply kwa wachina wa SGR

malembeka18

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2018
Posts
3,266
Reaction score
3,698
Habar wakuu wachina wa SGR weonyesha Nia yakufanya kazi na mim yakusupply then malipo utaratibu wao nibaada ya mwezi yaani unasupply Leo tar1 June tar 30 June Kisha malipo Yako yataanza kufanyiwa utaratibu July 1 pia malipo yanaweza kuchelewa still ukaendelea kuwasupply ...wakuu nauliza kwa mwenyewe uzoefu yoyote wa tenda za wachina wakoje na huu utaratibu wao
 
Mi nadhani kila ofisi ina utaratibu wake, hapo ni kuchunguza tu hao unaofanya nao kazi wapoje
 
Sitaki kusikia kuhusu SGR, mradi wa kitapeli sana huu. Tumefanya kazi yapi merzkezi mambo hayo hayo pesa ya toka Feb inapigwa kalenda kila siku leo unaambiwa hadi July
 
Sitaki kusikia kuhusu SGR, mradi wa kitapeli sana huu. Tumefanya kazi yapi merzkezi mambo hayo hayo pesa ya toka Feb inapigwa kalenda kila siku leo unaambiwa hadi July
Mkuu ndo wananiambia hivo kuwa utaratibu wao unasupply kwanza Hadi mwezi mzima uishe Kisha ndo wanaanza kufanyia taratibu za kukulipa pesa uku ukiendela kuwasupply japo hawajakulipa malipo ya mwezi uliopita Sasa huu utaratibu hakuna harufu yakupigwa kweli
 
Mi nadhani kila ofisi ina utaratibu wake, hapo ni kuchunguza tu hao unaofanya nao kazi wapoje
Uchunguzi sindo wengi husema huwa wasumbufu ktk malipo unapigwa karenda madai yawezi wa2 Hadi Sasa labda unakua hujalipwa nawanataka uendelee kwasuply uku wakiendela kukufanyia taratibu zamalipo yako
 
Kama hela yako ya mawazo au ya kukopa achana na huo mradi, huo nradi unataka watu wenye ukwasi mrefu, mfano

1june-30 june umessupply mzingo wa 300mil mamaake 1 july utatakiwa kusubmitt invoice ikiambatana na receipt ya efd daima receipt hiyo itakuwa na VAT ya almost 54mil, ambapo hiyo vat utakuja kufile august na utatakiwa kulipa,(hapo kama huna vat input mwezi husika. Itakapo fika hiyo august utakuta bado hujalipwa na hata ukilipwa wanaweza wakakulipa kidogo na sio yote wanaweza wakulipa hela ndogo kuliko hata unayodaiwa VAT.

Matokeo yake ni utaanza makimbizano na TRA, etc etc mambo yataanza kwenda zig zag.
 
Speaking from experience,

Niliwahi fanya kazi na wachina

wa mradi fulani hapa nchini,

nilikiwa nasupply mchanga

kwa ajili ya ujenzi wao na

kuwafyatulia tofali za block,

Makubaliano yalikuwa tulipane

kwa mwezi, kwenye upande

wa mchanga malipo yalikuwa

yanafanyika siku 15-18 baada

ya mwezi wa kazi kuisha.

Kasheshe ilikuwa kwenye

malipo ya tofali,

Wanakwambia wanalipa kwa

tofali walizochukua tu na

ambazo hazijavunjika, wakati

huohuo wanabeba na vipande

vya tofali, nilivyomaliza order

yao ya tofali ikabidi nitemane

na dili ya tofali nibaki na

mchanga pekee.

Kwenye mchanga tumeenda

vizuri kiasi, baadae siku za



malipo zikazidi kusogea

kutoka

siku 15 mpaka siku 20 mpaka

25 baada ya muda wa kazi

kuisha( mwezi)

Imebidi niachane nao kwanza

nikapoge dili za mtaani

angalau ninakuwa na

uhakika.

USHAURI :

kama una mtaji mkubwa

ambao hautegemei sana

malipo ili kujiendesha we piga

kazi nao maana kazi zao ni

endelevu,

Mimi imenibidi kuachana nao

kwanza kwa kuwa bado mtaji

wangu haujakuwa mkubwa

kivile maana kuna kipindi

mpaka naelemewa inabidi

nitoe pesa kutoka vyanzo

vingine ili kukamilisha kazi zao.

Jamaa hawadhulumu ila

malipo yao huchelewa

kidogo.



Nakutakia kazi njema.
 
Aiseee hao jamaa achana nao wasumbufu mnooo watakutia umaskini
Ndio uzuri wa JF, Penye wengi hpahalibiki jambo. malembeka18 nadhani umepata mwanga, sasa hapo ni jukumu lako kupambanua na kuchukua hatua.
 
Hizi biashara zinataka mtaji vinginevyo mtasumbuana tu.Shemeji yangu alifirisika kwa style kama hii alikuwa alipata tender hotel moja mjini hapa.

Waliingia mkataba wa kusambaza kuku 300 kwa mwezi,sukari na mafuta ya kula.Siku anakwenda fatilia anaambiwa manager hayupo kafanya wizi hivyo tumemuachisha kazi ndipo na haki zake zimepotelea hapo

Sent from my Infinix X656 using JamiiForums mobile app
 

Mkataba ulikuwa wa manager au hotel kaka maana mkataba ndio kila kitu
 
Mkataba ulikuwa wa manager au hotel kaka maana mkataba ndio kila kitu

Ndio ninashangaa yani meneja si aliingia mkataba kama custodian wa hotel? How comes useme afirisike kisa meneja amekufuzwa
 
Temana nao kuna jilani yangu alipata tenda kwao. Akaniomba ushauri nikamwambia temana nao hakuckia. Baaaana baada ya miezi 5-9 HOI kabisa. Full kukonda na sonona. Alitemana nao kwa hasara kubwa tu
 
Huyo shemeji yako alikuwa anauza kwenye kampuni/hotel au alikuwa anamuuzia meneja?na je kulikuwa na mkataba wowote au maandishi yoyote ya kuonesha amefanya supply hapo hotelini?
 
mkataba upo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…