Tendwa: Serikali ya mseto yanukia Zanzibar

Tendwa: Serikali ya mseto yanukia Zanzibar

Pdidy

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2007
Posts
57,951
Reaction score
32,619
Tendwa: Serikali ya mseto yanukia Zanzibar
broken-heart.jpg
Na Joyce Mmasi

MSAJILI wa vyama vya siasa nchini, John Tendwa amesema hatua ya Chama Cha Wananchi (CUF) kuitambua serikali ya Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Aman Karume ni hatua ya kuelekea kwenye Serikali ya Mseto visiwani humo.

Akizungumza na Mwananchi Jumapili ofisini kwake jijini Dar es Salaam wiki hii, Tendwa aliwapongeza Maalim Seif na Rais Karume kwa kufikia hatua hiyo.

Alisema, licha ya kuwa maridhiano hayo kuwashangaza wana CUF kwa vile hawakuyatarajia; hatua hiyo inafungua milango ya ushirikiano na sasa vyama hivyo vinaweza kuunda serikali ya pamoja baada ya Uchaguzi Mkuu ujao.

''Maridhiano hayo yatafungua milango ya kufikia muafaka kamili kwasababu sasa mazungumzo ya muafaka yataendelea na upo uwezekano wa kufikia suluhu la kudumu kwa vyama hivi kushirikiana kuunda serikali ya pamoja baada ya uchaguzi mkuu ujao,'' alisema Tendwa.

Tendwa aliwataka wafuasi wa CUF ambao hawajamuelewa Maalim Seif, wageuke na kumuunga mkono kwa kuwa aliyofanya yana manufaa kwao na taifa kwa ujumla.

Alisema hatua hiyo pia inafungua ukurasa mpya wa maelewano ya kisiasa kwa pande mbili hizo zilizokuwa zikipingana visiwani na hatimaye kuleta umoja wa Wazanzibari.

Msajili huyo wa vyama vya siasa alisema dunia ya leo ni ya majadiliano na masikilizano na kwamba, hiyo ndiyo njia pekee ya kutatua matatizo au tofauti zozote zizoibuka baina ya pande mbili zinazopingana au zinazogombana.

''Ni kweli ni mgeuko wa ghafla tena uliochelewa ...lakini ni msimamo chanya wa maendeleo na tunatarajia Watanzania wote sio wana CUF, wakiwemo Wazanzibari wataupongeza uamuzi huo na kuunga mkono, tusimtuhumu Seif ila tumpongeze na kumuunga mkono.

Akizungumzia hali ya kisiasa nchini, Tendwa alisema ni shwari na kwamba, migongano inayosikika katika baadhi ya vyama vya siasa ni ya kukuza demokrasia ndani ya vyama husika. ''Hayo unayoyasikia huko Chadema na CCM sio migogoro hata kidogo, ni migongano yenye nia ya kuboresha demokrasia katika vyama hivyo pamoja na kuimarisha hali ya kisiasa na uchumi wa nchi,'' alisema
 
Back
Top Bottom