Tenga: Jezi ni mali ya mchezaji si TFF

Bubu Msemaovyo

JF-Expert Member
Joined
May 9, 2007
Posts
4,120
Reaction score
3,468
Tenga: Jezi mali ya mchezaji Taifa Stars

Habari Zinazoshabihiana
• .... Jezi za 'Kikwete' zakabidhiwa TFF 04.01.2007 [Soma]
• Athuman Idd atafune jongoo kwa meno - Tenga 19.01.2007 [Soma]
• Tenga awapasha wachezaji Stars 13.09.2007 [Soma]

*Ampa tano Cannavaro kumvulia jezi Eto'o.

Na Erasto Stanslaus

RAIS wa Shiriksho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Leodegar Tenga amempongeza beki wa timu ya Taifa 'Taifa Stars', Nadir Haroub 'Canavaro' kubadilishana jezi na mchezaji wa kimataifa wa Kameruni, Samuel Eto'o katika mchezo wa marudiano wa kuwania kufuzu fainali za Kombe la Dunia na Mataifa ya Afrika 2010 uliofanyika mjini Younde, Kameruni.

Baada ya mchezo huo kumalizika 'Cannavaro' alifuatwa na Eto'o anayecheza klabu ya Barcelona ya Hispania akitaka wabadilishane jezi baada ya pambano hilo kumalizika ambapo Stars ilichapwa mabao 2-1 yaliyofungwa na mchezaji huyo.

Tukio hilo limeibua mjadala baada ya Ofisa Habari wa TFF, Florian Kaijage akikaririwa na vyombo vya habari akisema 'Cannavaro' atakatwa sh. 20,000 kwa kitendo cha kubadilishana jezi na Eto'o.

Mchezaji mwingine iliyeingia katika mzozo huo ni Jerry Tegete ambaye alibadilishana jezi na mchezaji Jean Makoun wa Kameruni anayevaa 11. Tegete alivaa jezi nambari 10 katika mchezo huo.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Tenga alikata mzizi wa fitina na kutoa ufafanuzi wa kina kuhusiana na sakata hilo na alimpongeza beki huyo akisema amefanya kitendo cha kishujaa kutoa jezi ya Taifa bila kujali kama atadaiwa au la.

"Canavaro amefanya kitendo cha kishujaa kwani sasa tunakwenda na wakati kwani angekataa kutoa jezi kwa kuhofia kudaiwa ulimwengu usingetuelewa na kutoa jezi ni kuitangaza nchi," alisema Tenga.

Nahodha huyo wa zamani wa timu ya Taifa, alisema kuanzia sasa TFF imepitisha uamuzi kila mchezaji wa Stars ataondoka na jezi aliyovaa siku ya mchezo bila kujali alicheza uwanjani au la baada ya pambano kumalizika na itakuwa mali yake.

Tenga alisema kimsingi waliokuwa wakimdai 'Cannavaro' jezi hiyo walikuwa wakitimiza wajibu waliojipangia kati ya uongozi wa Stars na wachezaji lakini alionya kuwa walishindwa kuangalia mazingira halisi ya tukio husika.

Baadhi ya wadau wa mpira wa miguu wameuponda uongozi wa TFF kutokana na kitendo hicho hicho na walikuwa tayari kuwalipia gharama za jezi hizo 'Cannavaro' na Tegete.
 
Hawa TFF nao mmh...

Tunashukuru kwa kufahamu ya ckwamba mliyokuwa mnaongea mwanzo ni aibu tupu...ati mwamdai mchezaji Jersey yake mwenyewe!!!

Bora mmefumbuka macho na kufahamu ya kwamba Dunia inabadilika.
 
Kauli ya leo toka kwa Leodger Chilla Tenga “kila mchezaji wa Stars, atakuwa anaondoka na jezi atakayoitumia kwenye kila mchezo hata kama atakuwa ni mchezaji wa akiba.”
 
Hivi hawa jamaa wa TFF wanamaanisha nini?? kaijage ni msemaje wa yale leodger na Mwakalebela wanayo amua hii kauli ni kweli au kajitoa kimasomaso kufuta aibu???
 
Thamani ya publicity tutakayoipta as nchi kwa mtu kama Etoo kuvaa jezi ya nchi yetu ipo juu sana ukilinganisha na hiyo elfu ishirini. I understand hii yote ni umaskini lakini basi ni vyema umaskini wetu ukawa na kikomo na kuishia kwenye mali tu na si fikra.
 
TFF wameona aibu wanajikosha baada ya wadau kuwazomewa na kushtukia kuwa watachunguzwa TAKUKURU) kwa ubadhirifu wa pesa za wafadhili pamoja na vifaa vya michezo vinavyotolewa na wadau mbalimbali wa michezo na wenye mapenzi mema na taifa stars

ama yawezekana wafadhili wamewakoromea kuhusu vifaa vyote wanavyotoa au wametaka.
 
Alafu jamaa hapo TFF nasikia wamejaza wenyewe tu kutoka kule kanda ya KASKAZINI MAGHARIBI na wadau wamewashtukia kwa hilo na wanasafishana wenyewe kwani hiyo ni AIBU yao
 
Hivi jezi hizo inakuwa sawa na mashuka ya gesti?
 
Hivi jezi hizo inakuwa sawa na mashuka ya gesti?


Kwa sisi tuliocheza mipira zamani wakati hari ya uchumi bado ni mbaya tunafahamu haya,kwamba jezi ni zaidi ya hayo mashuka ya gesti.
Unavua jezi unapotolewa kumpisha mwenzio aingie na jezi uliyo vaa wewe wakati huo huo.
Ndio maana zamani sio ajabu kukuta timu nzima ina ugonjwa wa UTANGO TANGO
 
Hapo umesema
 


Chanzo:
 
The Tanzania Football Federation (TFF) has reversed its decision to impose a financial penalty on a player who swapped jerseys with Samuel Eto'o.

Defender Nadir Haroub gave away his jersey to the Cameroon star after the teams' recent World Cup qualifier in Yaounde.

Tanzania lost a hard-fought encounter 2-1 and the local media praised Haroub and said his performance was the reason Eto'o was keen to swap jerseys with him.

But the TFF bigwigs were clearly not amused by the gesture and told Haroub that part of his allowance would be used to replace the jersey.

The team's management insisted that Taifa Stars players were not allowed to give away jerseys as the federation could not afford a new set of jerseys for each match.

But following criticism from the media and fans alike, the TFF has backtracked and said the player would not be punished.

"It's obvious he couldn't say no to Eto'o," said TFF president Leodegar Tenga.

"It was a wise decision to give his jersey to such a famous player. This will make our country known," he added.

A fund-raising drive was already underway with fans donating money to help Haroub meet the cost of replacing the jersey.
 


...Mkuu, Hujatulia! nimecheka!!!!!
 
....Yawezekana Kaijage anataka kutudisha....
 
Is shame to collect the jersey and reuse especially for the big game like that with Cameroun. If possible all the players should have changed tha jerseys with those of indomitable lions the image of african football. Is better to come back and pay rather than letting a golden chance of exchanging with Etoo to pass away. In one way or another you have advertised Tz outside there.
 
ukweli ni huu, walichotakiwa kufanya TFF ni kuitisha mkutano na waandishi wa habari kisha watueleze ni sababu ipi iliyopelekea timu kushindwa kufuzu kwa mara ya pili katika mashindano ya africa then kwa nini timu imeshindwa kwenda FNB south africa 2010, but walichokiona wao ni kuwa wakija na gea ya jezi wabongo hawatawauliza kwa nini timu haina maendeleo...na kama mlivyoona waandishi woote wakakimbilia ishu ya jezi na kusahau ile ya muhimu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…