Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
TENGENEZA SAFU IMARA; PEKEAKO HUTOWEZA!
Anaandika Robert Heriel
Mastermind!
Moja ya changamoto inayowakabili Vijana wengi ni kukosa SAFU nzuri au kukosa kabisa SAFU katika Maisha Yao.
Unakuta kakijana kawatu kapokapo tuu! Hakajui kaelekee wapi, hakajui kafanye nini, hakana watu walioupande wake.
Tatizo Hilo limeanzia mbali kidogo katika misingi ya Familia.
Familia ndio msingi Mkuu katika kuunda Safi ya kijana au Binti.
Sasa unakuta Baba na Mama walishaparangana, yaani SAFU Yao yenyewe imeshapanguka na kuvurugika.
Au unakuta Mama kapandikiza chuki kwa mtoto achukie Ndugu wa upande Baba au kinyume chake.
Unapokosa SAFU basi Maisha yako yapo katika hatari kubwa.
Taikon kama Mastermind, the game checker and Planner. Ninakuambia hivi leo. Ukiwa bado hujachelewa; TENGENEZA SAFU YAKO, Kwani Maisha pekeako hutoweza na hutofika popote.
Maisha kuna Wakati hayatabiriki Kutokana na Tabia na Akili ya Mwanadamu Kubadilika. Yaani wanaokuzunguka hivi leo uwaonavyo, hawatakuwa hivyo miaka 10 ijayo. Hata hiyo haina maana usipange Safu yako.
Maisha ni wewe, kisha ni wale unaohusiana nao jinsi walivyo.
Katika Vita kuna Safu za kivita,
Katika Siasa kuna Safu za kisiasa,
Katika Mpira wa miguu kuna Safu za wachezaji Mpira.
Katika ulinzi, mfano unapomuona Rais analindwa na wanausalama usidhani wamekaa hovyohovyo, wamewekwa Kwa Safu, yaani mpangilio maalumu Kwa sababu maalumu kulingana na uwezo na kazi ya mwanausalama husika.
Narefusha andiko sio?
Wazazi wetu pengine hawakutuachia Safu nzuri, Hilo lisitufanye tuwalaumu.
Huu ni Wakati wetu SASA.
Wakati wa kutengeneza SAFU bora katika mapambano ya kujikwamua kimaisha.
Usiishie kulalama, wala usiishie kusema Maisha ni bahati.
Ni kweli Maisha Wakati mwingine ni bahati lakini bahati hiyo inatokana na fursa iliyokutana na jitihada.
JINSI YA KUTENGENEZA SAFU BORA KUJIKWAMUA!
1. JITAMBUE.
Jielewe, jitambue wewe ni Nani, unahitaji nini kwenye Maisha, unauwezo gani, yapi mapungufu yako, yapi mapungufu yanaweza kufanyiwa marekebisho(yanarekebishika),
Ni ipi asili yako, na wapi unataka iwe Destination yako.
2. Tambua wanaokuzunguka.
Je ni Watu wenye mitazamo ipi juu yako,
Je wanaelewa nini kuhusu Maisha,
Je wanakuona katika Future ipi, je wanakutazamia utakuwa MTU wa Aina gani hapo baadaye,
Ni Kwa nini wanakuona hivyo, je ni kweli upo hivyo au ni vile uwezo wao wa Akili ulivyo au ni chuki au mapenzi yaliyopitiliza.
Elewa uwezo wa wanaokuzunguka,
Waweke Watu wanaokuzunguka katika Madaraja Yao,
Kunguru weka kwenye Banda la kunguru,
Njiwa weka kwenye Banda la njiwa,
Nguruwe weka kwenye Banda la nguruwe,
Sungura weka kwenye Banda lake.
Usiwaweke Watu kwenye makundi yasiyoyao, hiyo sio kwamba itawasumbua wao Bali itakusumbua wewe mwenyewe.
Watumie kila mmoja kulingana na Daraja lake, mfano, paka kwenye Banda la paka kazi yake ni kuwinda panya. Basi muweke kwenye majukumu yake/Safu yake
Usimuweke Paka kwenye Safu ya Mbwa.
Wote ni muhimu hivyo ni jinsi utakavyowatumia.
Elewa maslahi ya kila anayekuzunguka kwako, na maslahi yako Kwa kila unayemzunguka.
Usiwe karibu na MTU ambaye hujui nini anapata Kutoka Kwako na kipi inapata Kutoka kwake.
Hiyo ni dalili ya Ufa katika Safu yako.
Elewa kuwa shambulizi lolote katika mapambano huwa na athari kubwa endapo mshambuliaji akiwa karibu. Na mashambulizi mengi hutokea karibu zaidi.
Hata kwenye mpira, aliyekaribu na ndani Boksi la kipa ananafasi kubwa ya kuleta madhara tofauti na aliyenje ya Boksi la kipa.
Elewa uwezo wa wanaokuzunguka.
3. Yaelewe Mazingira.
Elewa utamaduni inayokuzunguka, elewa Tabia ya nchi na hali ya hewa, Soma mienendo ya Lugha za Watu na maana zake, Kwa kifupi ielewe Jiografia ya nchi au Dunia unayoishi. Elewa nini kipo wapi na kinapatikanaje, Nani wamiliki WA kitu hicho, elewa Michezo Michezo ya Mchana na Usiku. Usizubae zubae!
Fuatilia Historia ya Maeneo unayoishi na Yale yenye potentialities zako.
Ndio unapanga Safu hivyo. Ili ujue Nani akae wapi na afanye nini Kwa muda gani.
4. Weka Malengo, mipango na mikakati Kwa Yale utakayo kwenye Maisha.
Sasa unajijua ni Nani, uwezo wako, ushajua nini unataka katika Maisha, unawajua wanaokuzunguka, unajua mazingira. Kinachofuata hapo ni kuseti malengo, mikakati katika kutimiza like unachotaka kwenye Maisha.
Mfano 01; Lengo: Nataka kuwa Msanii WA muziki.
i. Mimi ninataka kuwa msanii wa muziki Kwa sababu napenda muziki lakini pia ninakipaji cha kuimba.
ii. Sina mazoezi ya kutosha, pia sina maarifa ya kutosha kuhusu muziki kwani sikuusomea, ninajua tuu kuimba.
Mkakati; Nitaweka Ratiba ya mazoezi ya kuimba angalau kila Siku masaa mawili. Lisaa limoja Asubuhi, kisha lisaa jingine jioni. Yatakuwa ni mazoezi ya Sauti.
Kwa vile Kwa sasa sina Pesa za kuajiri mwalimu nitajifunza kupitia mtandao, pia nitaenda kujiungamanisha na vikundi vya waimbaji hata kama ni kwaya za kanisa nitaenda. Huko nitapata ujuzi kidogo.
iii. Ninaaibu na sijiamini Hii NI Kutokana na baadhi ya wanaonizunguka kuniambia siwezi kuimba, wananikatisha tamaa.
Mkakati; Baada ya kufanya mazoezi Kwa miezi mitatu mfululizo nitaanza kuimba Mbele ya wakosoaji wangu ili Kupata Maoni Yao. Lazima nikubali kukosolewa na nijitahidi kuhimili maneno Yao. Hii itanisaidia kuwa imara, kuondoa aibu na kujiamini kwani nitakuwa ninawazoea na nitazoea kukosolewa.
iv. Hakuna anayeamini katika kipaji changu, na hakuna anayenijua. Sina jina kubwa.
Mkakati; tayari ninazingatia mazoezi na ninazidi kuimarika, tayari ninazoea ukosoaji wa mashabiki wasionitaka au pengine wanaotaka niwe Bora. Aibu inaondoka na kujiamini kumeongezeka, angalau sasa nimepata uzoefu kidogo.
Nitaanza kujitangaza Kwa kuomba kuimba kwenye matukio mbalimbali iwe ni harusi, sherehe, misiba, Kanisani iwe hata Kwa kujitolea. Na Hii ni kujenga msingi wa kujitangaza.
Hii itafanyika Kwa angalau nusu Mwaka mpaka miaka miwili.
v. Tayari Watu wa eneo Hili wameshanijua. Jina langu limekua na kipaji changu ninazidi kuchanja mbuga. Nataka nijulikane kitaifa.
Mkakati; nitatumia mitandao ya kijamii kujitangaza na kutangaza kipaji changu.
Nitaomba Interview kwenye media mbalimbali. Kisha nitajitahidi kujiweka karibu na wasanii ambao wanafahamika waliokwisha kunitangulia.
Safu ya wasanii nitakayoichagua itatokana na kile ninachokitaka kitokee hapo baadaye.
Tuachane na mambo ya muziki.
Upangaji wa Safu unahusu Maisha yako mwenyewe.
MTU yeyote akitaka kuona future yako basi kitu cha Kwanza atakuangalia wewe kisha Safu yako ni kina Nani yaani upo na Nani katika mchezo wako.
Na MTU yeyote ambaye anataka kukudhuru wewe basi atakutazama wewe kisha aangalie Safu yako inayokuzunguka, anaweza Kutumia Safu yako hiyohiyo kukupiga na kukushinda au anaweza kutumia Ufa uliopo katika Safu yako.
Watu utakaowachagua katika Safu yako itakupasa uwe nao Makini Sana. Kwanza waelewe ili wasikupe shida au wasijemrahisishia adui yako kukupiga.
Katika hiyo Safu uliyoiweka hakikisha unajua nini chakusema Kwa kila Safu unayoingia.
Usijeenda kwenye Safu ya Mbwa ukaita Mlio WA paka Tchi! Tshi! Tchi! Nyau!nyau! Utakwama.
Au usijeenda kwenye Banda la Njiwa alafu ukaita Mlio WA kuita Kuku, kukukuku! Pba!pba!papa!
Be smart! Elewa kuwa kila MTU na kila Safu inalugha yake na uchezaji wake na kazi yake.
Wewe ushajua MTU ni mbeya, Hana Siri na bado unamwambia mambo yako. Alafu unamlaumu na kumtukana kuwa ni Mbaya na mnafiki. Wewe ndio mjinga uliyeshindwa kujua yupi asikie nini na Nani asikisikie nini katika Safu yako.
Katika utengenezaji wa Safu, usipende kugombana na watu endapo wataenda kinyume na vile ulivyowapanga, elewa kuwa kuna Leo na KESHO. Leo anaweza kuboronga lakini kesho anaweza kufanya vizuri.
Hakikisha katika Safu kuna wachezaji Sub. Kwamba huyu akizingua basi unampumzisha Kwa muda atafaa Kwa MATUMIZI YA baadaye. Ndivyo mambo yanavyofanyika.
Elewa kuwa kuunda Safu nayo ni kazi ngumu zaidi hasa Kwa Vijana ambao wametoka familia masikini.
Kufanya usajili WA wachezaji wenye uwezo inahitaji uwezo wa kifedha, kipaji kikubwa au Elimu Fulani ya kipekee.
Taikon nipumzike SASA
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam