The Tai
Member
- Dec 9, 2019
- 6
- 15
PESA NJE YA AJIRA.
Wapo watu wengi ambao wanashindwa kufanya biashara japokuwa wana mitaji ya kutosha na hii inatokana na sababu ya kwamba wanakuwa wametingwa na ajira zao.Pale wanapojaribu kufanya biashara mara nyingi huangukia pua na kupata hasara kwa sababu ya biashara zao kukosa usimamizi wa karibu .Leo naomba nikupe mfano ambayo unaweza utumia ili kuingiza pesa wewe mwenye mtaji lakini unakosa muda wa kusimamia biashara yako.
Ukipata nafasi zunguka mtaani kwako nashani utaona asilimia kubwa wanaotuuzia vitafutio ni kina mama na ukijaribu kupiga nao soga kidogo kuhusu biashara zao utagundua wengi wanatamani kupanua biashara zao ili auze zaidi
Mfano anauza maandazi lakini anatamani auze chai,auze na chakula cha mchana.Ari na vifaa anavyo lakini hana mtaji.
Unaanzaje sasa?
Tafuta wamama watano mtaani kwako (wasiwe wanakaa karibu karibu) ambao wanauza vitafunio asubuhi na hawana mitaji ya kuongezea.Hao wamama/wadada uwe unafahamiana nao vizuri na kama hufahamiani nao vizuri basi jaribu kuwafatilia kwa kuwachunguza ikiwemo tabia zao ili ujue namna ya kuwaingilia.
Baada kuwapata hao wanawake watano mfate kila mmoja kwa muda wake muelezee kwamba wewe umpe mtaji wa laki moja yeye apanue biashara yaani kama alikuwa anauza maandizi tu aongeze na supu,chai,chapati,chakula cha mchana n.k katika huo mtaji matarijio ya chini ya faida ni Tsh 10000 yaani asilimia 10 ya mtaji.
Hivyo basi umpe mtaji kisha mtakuwa mnagawana faida wewe unachukua elfu tatu yeye anachukua faida inayobaki kwa siku(hata ikiwa zaidi kutokana na makubaliano yenu) na kumbuka hapo mwanamke anatoa nguvukazi,vyombo na muda wale wewe unatoa mtaji basi.
Baada ya hapo sharti ni kwamba msaini mkataba usiopungua siku 100 yaani aqe anakulipa Tsh 3000 kila siku kwa siku mia na huo mkataba mnasaini kwa mwenyekiti wa mtaa na kila mmoja na shahidi yake.
Sasa kumbuka hapo umewasainisha wanawake watano na kwa kila mmoja baada ya siku mia utakuwa umejikusanyia kiasi cha Tsh 300000 kwa wamama watano utakuwa na jumla ya Tsh milioni moja na laki tano ukitoka mtaji wa laki 5 unabaki na faida ya Tsh milioni moja. Sasa baada ya hapo mkataba kuisha utaamua wewe uhame utafute mtu mwingine au uendelee naye ila nashauri kama utaamua kwenda kwa mwingine ule mtaji umuachie tu kama zawadi usiuchukue.
Hapo ndugu yangu utakuwa umemsaidia yule mtu kujiongezea kipato maana ana familia,ana michezo ya kinamama pamoja na vikoba na wewe utakuwa umejiongezea kipato bila wewe kushiriki moja kwa moja huku unafanya mambo yako mengine.
Mfumo huu wa biashara nimeufanya mara mbili na umenilipa.Niliwahi kushirikiana na rafiki yangu niliyesoma nae high school ifunda technical secondary school.Sisi tuliwatumia wale wamama wanaouza vitafunio shuleni na yule mama alikuwa anatulipa elfu tano kwa siku kwa sababu shule ilikuwa kubwa wanafunzi zaidi ya elfu moja hivyo ata faida ilikuwa kubwa na tulimpa laki moja tu na kizuri zaidi hata hatukusaini mikataba tulitokea tu kuaminiana.
Mara ya pili nimefanya mimi peke yangu baada ya kumaliza kidato cha sita mfukoni nilikuwa na laki sita niliyochuma nikiwa shule.Likizo nilienda morogoro mtaa wa mafisa pale nilifanya aina hii ya biashara na imenivusha mahali kwa kiasi fulani si haba.
USHAURI.
Kama utapenda kufata mfumo huu wa biashara fanya yafuatayo.
1.Wewe uwe mteja namba moja unaweza kutenga siku za kwenda kuwaungisha hapo kina mama kila mmoja na siku yake.
2.Usile chakula kwa mkopo lipa kabisa ata kama unajua baadae utaletewa hela yako.
3.Ukiwa nae usipende kumzonga kuhusu biashara hiyo wewe mpe uhuru wa kufanya anavyoona ni sahihi muhimu tu haingilii masilahi yako.