Tengeneza upekee na umuhimu uchaguliwe kundini

Tengeneza upekee na umuhimu uchaguliwe kundini

Joined
Nov 6, 2016
Posts
77
Reaction score
271
TENGENEZA NAFASI, ILI UWE MUHIMU NA UCHAGULIWE KUTOKA KUNDINI

Na Comrade Ally Maftah

Somo la leo nitajumuisha maeneo yote ninayofanyia kazi kwa ukaribu na uzoefu wangu tangu naanza kazi mpaka leo nilopofanya maamuzi ya kutoajiliwa tena isipokuwa kwa mkataba wenye maslai mapana mno.

Moja ya kasoro ninazoziona kwa vijana ni kushindwa kutengeneza nafasi ya upekee na ufanisi katika unachokifanya au kukiamini. kuna kauli ya bosi wangu ambae kwa kweli kwa wakati ule sikuwa namwelewa na nilitengeneza hisia kwamba alikuwa akinichukia Dada huyo alikuwa na kariba ya ukali na umakini katika ufuatiliaji tukiwa kampuni moja kubwa la vinywaji baridi duniani, ambalo lina ofisi zake mikocheni, nilikuwa afisa mauza katika hotel, bar na restaurant maalumu na maarufu Key Account Outlet,, alikuwa akisema ukifanya kawaida utalipwa mshahara wako, ukifanya zaidi utapata zaidi, kwa kipindi hicho umri wamgu ulikuwa mdogo, sikuweza kumwelewa aliye mwelewa ni rafiki yetu mmoja ambae alifanya ziada alituzidi nafasi kwa haraka, tukaanza kupata hisia za wivu tukijiona tuna elimu kubwa kumbe hatukuwa na tija kubwa kwa bosi, line meneja wetu.

NINI NILICHOJIFUNZA
Jitahidi kwenye kila unachofanya ujenge nafasi ya kipekee kwa kuwazidi wenzako au kwa kujitofautisha katika ubora, hiyo ndio njia pekee inayoweza kukusaidia kupata nafasi ya ziada, ukiachana na suala la bahati.

Ukiacha wanaopata nafasi kwa bahati, wengine wote hutengeneza mazingira ya kupata kukwezwa, ukiacha MUNGU nafasi zinagawiwa na binadamu wenzetu, sasa wewe umewezaje kumshawishi mtu akupe nafasi wewe katika dunia yenye watu bilion 8 na zaidi?

MAKALA IJAYO NITAELEZA NAMNA YA KUTENGENEZA NAFASI

NDIMI
Comrade Ally Maftah
JITU LA MIRABA
KING OF ALL SOCIAL MEDIA
 

Attachments

  • 2024-05-27-171619187.mp4
    8.6 MB
Back
Top Bottom