City centre. Kwa watu wenye akili public transport inaanzia in the heart of the city. Private cars ndio wanatumia mbinu tofauti kuziondoa katikati ya jiji.Mkuu vipi kuhusu intercity buses zinaanziaga wapi?
Kutokana na uzoefu wangu binafsi, naona wako sahihi kuweka station ya SGR kule City Center, wako sahihi kabisa kuhusu hilo. Isipokuwa tatizo lipo kwenye Designing ya mtandao wa reli yenyewe. Reli kwa Treni za namna hiyo nimeona aidha ziwe za juu, Yaani katika maeneo ya mijini kulikojengeka sana treni inapita kwenye madaraja ya juu (overhead bridges) na hata stations zake zinakuwa huko huko juu kwenye majumba ya ghorofa au treni hizo zinapita chini ya Ardhi kwenye handaki (underground railroad) na stations zake pia zinakuwa huko huko chini ya Ardhi kwenye mahabdaki. Majengo ya stations yanakuwa na lift za Watu kushuka au kupanda. Walichokosea SGR hii ya kwetu ni Designing ya Ujenzi wa Reli yenyewe, kwa sehemu kubwa Sana reli ya SGR imepita kwenye usawa wa Ardhi (on the Land surface), kitu ambacho Siyo sahihi hususani kwenye maeneo ya mijini Kama Dsm kwaw sababu inaingiliana na shughuli zingine za binadamu.Habarini wana jamvi.
Wakati ujenzi wa reli ukikaribia kuzinduliwa kwa route ya Dar es Salaam - Dodoma
Hivi ulishawahi kujiuliza wasomi wetu waliwaza nini kutengeneza daraja kubwa kuanzia vinginguti mpaka posta?
Unaweza piga hesabu pesa kiasi gani imetumika ili treni ifike tu posta?
Nazungumzia treni ya abiria usijesema ina link na bandari ili ipakie mizigo toka bandarini.
Vipi kwani treni hii isingeanzia gongo la mboto. Ikatengenezwa stand maridhawa na abiria wangeenda abiri huko badala ya kuja mpaka posta?
Hivi nia ya kuhamisha stand ya mabasi ya mikoani toka mnazi mmoja mpaka ubungo na hatimaye mbezi lengo lilikua nini haswa?
Najua jf ina wasomi hodari wataweza kuniondolea hili dukuduku langu la kutaka kujua kwa nini sgr ianzie city center tena kwa kujengewa daraja kubwa toka vingunguti, badala ya kuondoa msongamano na kujengewa nje ya mji.
Asanteni.
umemaliza kila kitu mkuu.Tumeondoa bus terminal Kisutu, Mnazi mmoja na Msimbazi kwa nia ya kuondoa msongamano wa magari katikati ya jiji.
SGR ina njia inayojitegemea.