Jamani eti mfanyakazi akifanya kazi miaka sita halafu mwajiri akasetisha mkataba haki zake Ni malipo Gani ukiacha nssf au ppf. Akipunjwa afanyeje ili kudai haki yake? Please help
Ni vizuri utafute mwanasheria akueleweshe zaidi, lakini kwa uelewa wangu mfupi na umepunguzwa na muajiri wako, muhimu ni haya;
1. Inatakiwa kikao cha wafanyakazi wote akiwemo muajiri ili kujulishana hali na mstakabari wa kampuni
2. Inatakiwa mpewe barua ya kuwajulisha wafanyakazi wote miezi mitatu kabla ya zoezi la kupunguza, pia hii barua inaweza kuandikwa na kubandikwa ubao wa matangazo ambao kila mfanyakazi ataisoma.
3. Baada ya miezi mitatu, wafanyakazi waliopunguzwa inatakiwa kila mmoja apewe barua yake ikiainisha sababu za kupunguzwa
4. Baada ya kupata barua, inatakiwa muajiri akae na nyie kikao ili kuwapa taarifa kamili, ushauri, na namna ya kusaidiana
5. Baada ya hicho kikao inatakiwa kila mfanyakazi kwa wakati wake wakutane na uongozi ili kuongelea malipo yako, utalipwa miezi mingapi na kwanini wakulipe miezi hiyo.
NB: Sheria ya nchi ya ajira inasema mfanyakazi akiajishwa kazi kwa sababu zinazohusu kampuni inatakiwa ulipwe miezi 12