Habari za kazi!
Kuna mfanyakazi alipata ajali lakini nje ya ofisi. Alikuwa position ya mlinzi, sasa alipewa likizo ya kuumwa ya siku 126 kama sheria ya ajira inavyosema. Siku zimekwisha lakini Inavyoonekana bado hayuko katika hali nzuri kwani mkono uliwekewa chuma na hivyo itakuwa vigumu kwake kufanya kazi hasa katika nafasi hiyo ya mlinzi.
Nauliza ni procedure gani zinapwa kufuatwa kama unataka kumuachisha kazi kwa sababu za kuumwa? Asanteni na nitafurahi kwa ushauri.