Kuweni makini na hawa wanaosemekana kupata maono na kuwaletea shuhuda zao.
Ukiwafuatilia hawa wote wanaoleta hizi shuhuda utapata mikanganyiko mingi sana.
Wao hudai walikutana na Nguvu za Mungu na wanatusihi tuokoke lkn chaajabu yale waliyokutana nayo huko ktk maono yao yanakinzana na Maandiko ya biblia wanazotusihi tuzisome.
Mfamo huyo jamaa anasema ukifa ni hukumu lkn Biblia anayotusihi tuisome inasema ukifa hakuna liendelealo ni usingiz mpka siku ya hukumu ya pamoja yaan ufufuao wa watenda mema na baadae ufufuo wa watenda maovu watakapo hukumiwa pamoja na shetan.
Pia jamaa anasema alifufuliwa baada ya kufa kwa kitambo lkn biblia inasema huwez kufufuka mpka Ufufuo wa Yesu, je huyo jamaa huoni anapingana na imani yake?
Pia ukifuatilia shahidi za watoa ushuhuda wanaosema walipitia mambo kama ya huyo jamaa utagundua wote wana stori zinazokinzana.
Yaan huyo anasema alikutana na yesu yuko hiv, mara mwngne atasema alikutana na yesu yuko vile, mwingne anasema alikuwa kuzimu kwa kupata cheo cha umalikia wa kuzimu kwa muda fulan, wakati huo huo ukisikiliza shuhuda za mwingine atakwambia ane alikuwa malikia wa kuzimu kwa muda fulan, je tumuamini nani na tumuache nani?
Na kuna hii kasumba ya watoa shuhuda kusema kwamba alipokuwa mshirikina alisababisha ajari sehemu fulan na kuuwa watu kiasi fulan, lkn ukienda kuchunguza hiyo ajar utakuta kumbe chanzo chake hakileti maana kuwa kilisababishwa na nguvu za giza, pengine ulevi, miundombinu mibaya, uzembe, haiishii hapa pia ukimsikiliza mtoa shuhuda mwingine anaesema alikuwa mshirikina utamsikia nae akiitaja hiyo ajari kuhusika nayo, wakati huo kuna mwingine ulimsikia alisema alihusika na hiyo ajari JE TUMUAMINI YUPI?
Yaan jambo moja limetendwa na watu tofaut kwa sabbu tofaut na kila mtoa shuhuda na mambo yake, yaan hawatoi shuhuda za kumake sense.
KIUFUPI ni kwmba kuna viumbe ambao kazi yao ni kuwapagaa watu kishirikina na kuwapa Maono ya uongo kuhusu MUUMBA, pia kuwafanyia mazingaombwe ya akili kwa kuwahadaa kuwakutanisha na Yesu sjui malaika huu ni uongo.
Nyakati zetu hakuna na hakuna aliyewahi kukutana na malaika akaishi, na hatuna nguvu wala uwezo wa kwenda mbingun, zaidi ya hayo mazingaombwe na mashuhuda ya wahuni waliopagawa na pepo, kuja kutuletea Vitisho vya kipumbavu.
Huyo jamaa yenu aliyeishi miaka1000 mleteni tumtandike maswali ya ufahamu na uwakika hawezi kuyajibu maana alipagawa kwa kufanyiwa mazingaombwe ya maono ya uongo, hayo maono ya mashetan ndyo wanayowapa wachungaji zenu makanisan na misikitini.
NARUDIA TENA kizaz chetu hakuna aliyewai kumuona kristo, hakuna aliyewai kumuona malaika wa kwel, achana na hayo mashetan yanayojibadili tabia kujifanya NURU kumbe ni giza, hakuna aliyewai kwenda mbingun na hakuna aliyepo Motoni kuungua maana HUKUMU bado muda wake haujafika, hao mnaosimuliwa wapo motoni ni Maono ya uongo mnayopewa na mashetan ambayo ndyo huongoza harakati za manabii wa Uongo na Chapa ya 666.
Acheni kuogopa, Moto haupo wala jehanam hakupo kama mnavyotishwa, Chamuhimu tenda mema na Uamini Kuna Muumba FULL STOP ajuaye maisha baada ya kifo ni MUUMBA PEKEE NA ALIYE KUFA TU, NA SI MWINGINE, hata shetana na Nguvu alizo nazo hana ubavu wa kukuamulia pa kwenda baada ya kufa na hana ubavu wa kukufufua labda kama ulikufa kimazingara.