Tetesi: Kocha Mchezaji anawabania wenzake huko South

Greatest Of All Time

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2017
Posts
23,620
Reaction score
52,790
Kuna tetesi zinasambaa kuwa mtangazaji maarufu kama kocha mchezaji anawabania wenzake wasitangaze mechi za kombe la dunia kwa kiswahili huko south afrika.

Ikumbukwe takribani watangazaji sita wa kitanzania walikula mkataba wa kutangaza kombe la dunia kwa kiswahili kutoka bondeni kwa madiba.

Lakini mara baada ya mechi za makundi kuisha, wanaotangaza mechi mara kwa mara ni kocha mchezaji na mzee wa kaliua huku mara chache sana akisika mzee wa jahazi.

Baadhi ya watangazaji na wachambuzi ambao wamepigwa benchi kiaina na hawasikiki kabisa ni pamoja na Mzee wa mwanaspoti, Mzee wa hisabati a.k.a kiungo mkongwe pamoja na mtangazaji mwingine nguli wa siku nyingi.
 
Kwani kitenge ndo aliyepewa jukumu la kuwachagua hao macommentetor?
 
Hii thread mbovu kuwahi kutokea tangu jamii forums ifunguliwe
 


Binafsi sishangazwi na taarifa kama hii, kwani sisi watanzania kwa majungu ndio wenyewe...waliotoa taarifa hizi bila shaka ni hao wanaodaiwa kubaniwa na kocha mchezaji...nchi hii imejaa majungu sana...tabia yetu watanzania na ambayo tuna sifa nayo katika eneo hili la Afrika mashariki na kati ni ile ya majungu na fitina...tunaogopwa kwa hilo au hili...watanzania sisi ni wanafiki na wapiga majungu sana...yaani kazini ni majungu, mitaani ni majungu, kwenye familia ni majungu, kwenye siasa ni majungu, kwenye kichezo ni majungu na fitina..mradi kila mahali ni majungu na fitina tu
 
Huyo kocha mchezaji ndo director of Human Resource and Administration hapo Supersport?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…