Greatest Of All Time
JF-Expert Member
- Jan 1, 2017
- 23,620
- 52,790
Kumekuwa na tetesi nyingi mitandaoni juu ya hatma ya Mshambuliaji na Nahodha wa Taifa Stars Mbwana Samatta "Popa" ambaye anaweza akawekwa sokoni na kuuzwa muda wowote kuanzia sasa.
Hayo yamezuka mara baada ya Villa kumsajili mshambuliaji Ollie Watkins kutoka Brentford kwa ada ya Pauni Milioni 28 na pia wapo katika mipango ya mwisho ya kumsajili mshambuliaji Joshua King kutoka kwa washuka daraja Bournemouth.
Endapo Joshua King atatua Villa, Samatta atakuwa sokoni huku Bekistas ya Uturuki ikimuwania kwa udi na uvumba.
Villa wanekuwa busy sokoni wakisaka sajili mpya, ili kuepukana na kadhia ya msimu uliopita, ya kusubiria hadi siku ya mwisho ya msimu ndio wasalie ligi ya primia.
My take:
Vyovyote itakavyokuwa Samatta ameshaingia kwenye vitabu vya historia ya Nchi hii, kama miongoni mwa mashujaa wake katika suala la michezo!