Tetesi: Samatta anaweza kuuzwa na Aston Villa muda wowote kuanzia sasa

Greatest Of All Time

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2017
Posts
23,620
Reaction score
52,790
Kumekuwa na tetesi nyingi mitandaoni juu ya hatma ya Mshambuliaji na Nahodha wa Taifa Stars Mbwana Samatta "Popa" ambaye anaweza akawekwa sokoni na kuuzwa muda wowote kuanzia sasa.

Hayo yamezuka mara baada ya Villa kumsajili mshambuliaji Ollie Watkins kutoka Brentford kwa ada ya Pauni Milioni 28 na pia wapo katika mipango ya mwisho ya kumsajili mshambuliaji Joshua King kutoka kwa washuka daraja Bournemouth.

Endapo Joshua King atatua Villa, Samatta atakuwa sokoni huku Bekistas ya Uturuki ikimuwania kwa udi na uvumba.

Villa wanekuwa busy sokoni wakisaka sajili mpya, ili kuepukana na kadhia ya msimu uliopita, ya kusubiria hadi siku ya mwisho ya msimu ndio wasalie ligi ya primia.

My take:
Vyovyote itakavyokuwa Samatta ameshaingia kwenye vitabu vya historia ya Nchi hii, kama miongoni mwa mashujaa wake katika suala la michezo!
 

Sawa lakini umri ulimruhusu KDB
 
Watanzania wamelaani hamna kitu!kwa hali hii Samartta ataonyesha lini "umahiri" wa kulisaka kabumbu?...kila siku yupo mnadani kama sox za mitumba

Mbona kwenye maisha ya soka ni hali ya kawaida, Balotelli kila siku anazuruta kwenye timu mpya, zamani alikuwepo Nicolaus Anelka kila misimu miwili yupo kwenye timu mpya
 
Ila na yeye abadilishe mfumo wake sasa wa uchezaji. Tangu asajiliwe kwenye hiyo timu ya Aston Villa amekua akicheza 'kinyonge' sana!

Hata kama ndiyo maelekezo ya mwalimu, bado alitakiwa ajiongeze. Muda mwingi unamkuta anatembea tu uwanjani. Huoni akipambana kuwapangua mabeki, kupiga mashuti hatarishi, nk.

Sijui ni kwa sababu ya mwili wake mdogo!!
 
KDB Sio bora tu EPL bali Duniani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…