Tetesi:sasa wachezaji wa kigeni kua 7! msimu ujao!!!

Tetesi:sasa wachezaji wa kigeni kua 7! msimu ujao!!!

Wonderful

JF-Expert Member
Joined
Apr 8, 2015
Posts
7,347
Reaction score
5,986
Wakuu.
Taarifa za chini ya kapeti zinasema kwamba lile ombi la Yanga la kutaka waruhusiwe kusajiri wachezaji 8 wa kigeni limekubaliwa kiaina ila TFF na kamati zake imepunguza na kubaki saba.
Tutaendelea kujuzana hapa ndani,na
kila mwenye taarifa rasmi aiweke hapa pia.
 
Taarifa njema kwa club za yanga na azam ambazo zitashiriki mashindano ya kimataifa.
 
Hata waruhusu wote tu ni Sawa!! Sana sana itawafaidisha Simba, Yanga, na Azam... Ambao ndio wauwaji wazuri wa vipaji vya wachezaji wetu.
 
Hapa ndo huwa nashindwa kuwaelewa watawala wa soka letu, sasa hili suala wanasubiri lini kuamua/kutamka wakati usajiri ushaanza? Mbona waliingiza sheria za mchangani kwenye ligi harakaharaka lakini hili la muhimu wako kimya?
Enyi tff wapeni watu vitu....
 
Wangeruhusu tu hao 8 wasajiriwe halafu wakaweka kanuni kwamba kwenye ligi au mashindano ya ndani mwisho 5 kupangwa kwa pamoja kwa mechi moja
 
na sisi simba je

Ninyi Simba SC ni wa mchangani, hamuwezi kuwalipa wachezaji hao, endeleeni kujenga timu yenu ya vijana - zoezi mlilolianzisha tangu 2011 hadi sasa.

Updates: Imependekezwa wachezaji wawe 10 siyo 7.
 
Ninyi Simba SC ni wa mchangani, hamuwezi kuwalipa wachezaji hao, endeleeni kujenga timu yenu ya vijana - zoezi mlilolianzisha tangu 2011 hadi sasa.

Updates: Imependekezwa wachezaji wawe 10 siyo 7.

TFF, Wizara ya elimu na wizarainayoshughulikia michezo wakitaka kuelewa madhira yanayoipata michezo yetuwafanye utafiti ambao inabidi uhusisheuchunguzi wa mwenendo na maendeleo ya michezo yetu kabla na baada ya uhuru, halafu baada yauhuru, mabadiliko ya mifumo na sera za uchumi kuanzia Ujamaa, Kilimo cha kufana kupona, elimu ya kujitegemea na kubana na kuchangia gharama mpaka ile yakufuta michezo mashuleni. Wataweza ku confirm kwamba wakatibaadhi ya sera zilisaidia maendeleo na utendaji mzuri kwenye sekta hii, lakinikwa ujumla:
  1. tumeanguka ukilinganisha na miaka ya mwanzompaka miongo miwili baada ya uhuru ambapo watabaini kuwa tumekwisha katikamichezo karibu yote kwa performance
  2. Ushirikikatika michezo yote ukiacha mpira wa miguu na kikapu, imebaki kwenye vyombo vyadola pekee
  3. Siasa ya ujamaa ilisaidia kidogo kwa mashirikaya umma kwa kutengeneza ajira kwa vijana tukapata timu kama pamba, tumbaku,pilsner, sigara, RTC n.k lakini zisingedumu ajili ya utawala bora ktk kuendeshamashirika ambao ulibadilishwa na ubinafsishaji ambapo wamebaki kina AZAM naSukari kwenye gemu Zaidi kwa kuwa ni wazalendo. Wawekezaji wengine na penginewakubwa Zaidi hawashiriki.
Maelezo ya hapojuu ni kuwa, utendaji mzuri kwenye michezo miongo 2 baada ya uhuru ilitokana naviongozi au wachezaji ambao aidha walikuwa waalimu au wanafunzi wakati waukoloni, na kwa bahati, wanafunzi wa wanafunzi wa enzi hizo. Ndiyo maana;
  1. Boxing walimaliza akina Titus Simba, Kinyogoli,Mzee Matumla, Msomba, Isangura n.k miakaya 1970 na 1980
  2. Riadhaakina Bayi, Nyambui, Mosi Ally, Mwinga Mwanjala na NZAELI KYOMO Phase 1 miakaya 1980 mwanzoni na Phase 2 ya marathon ikaenda na Ikangaa. Juzi akina Bayiwana peleka wanafunzi Eldoret kwenye training unaona huruma wanaonekana kabisahawana furaha.
  3. Sokawalimalizia akina Aluu Ally, Niko Njohole, Thuweiny Ally, Kuka na akina Kulagwaupande mmoja, akina Adolph, Tino, pondamali, mkweche et.c upande wa pili nakidogo akina yanga bwanga bila kuwasahau akina mahadhi na mambosasa Phase I,Phase II na III kidogo akina China, Chambua, Kizota, Masatu, Marsha, GagaMogela et.c. Baada ya hapo tumepotea. Hizo Phase Iand ii zina uhusiano wa karibu wa mfumo wa elimu tuliyorithi na initiativeszetu ambazo hata kama zilikuwa na faida zimetudhuru. Tathmini ya ndani inaweza kuchambua mengihata maeneo ya taifa hili yenye uwezo wa kutoa wanamichezo bora kwa mfano:

  1. MBIO FUPI Mbeya, kidogo Iringa
  2. Mbio ndefu, Iringa, singida, manyara
  3. Ngumi; Kilimanjaro n.k
Muundowa wizara pia uangaliwe vizuri, hii sekta irudi kwenye elimu na tuondokane nadhana kuwa michezo ni hobby badala ya kuwa eneo la kitaaluma. Shule zifanye mambo makuu matatu:taaluma za darasani na vitendo, michezo, ujasiriamali. Ukaguzi wa elimu uwe endelevu na tuzo kwawanaofanikiwa na adhabu kwa wazembe zizingatiwe. Baadaya miaka 5 nchi itabadilika, na mambo ya kulilia idadi kubwa ya wachezaji wanjeyataisha.
 
Wadau wa soka na watz wenzangu nina mtizamo, nianze na swali kwanza. Ni wachezaji wangapi wa kitanzania wanacheza vilabu vya Uganda, Rwanda, Burundi na Kenya? na ni wachezaji wangapi toka hizo nchi majirani zetu wanacheza hapa kwetu? jibu ni moja, wanakuja kuliko sie tunavyokwenda. Ni nini sasa kinasababisha?

1.Hatuna wachezaji wengi wenye viwango vya kuwashawishi wenzetu. Na ndo maana utaona wanaturuka sie na badala yake wanaamua kwenda nchi zenye wachezaji wenye uwezo na vipaji kuliko wale walionao wao mf.Zimbabwe,Zambia,Sudani,Ethiopia n.k 2.Wachezaji wetu si washindani wa mafanikio. Wenzetu ni watu wa kutafuta mafanikio na kujituma sana, wakati wenzao wanacheza kazi kazi sisi wa kwetu wanacheza like for funny,show game bila kujali matokeo. Sasa hata tukisema tuzuie mapro, kimsingi haitawasaidia watu wa hivi badala yake itawaumiza Yanga ambao katika mashindano yao wanakutana na timu zinazoundwa na mapro wa maana kutoka nchi kibao.Tuelewe sahivi mpira ni kazi na ajira, kuwabeba wachezaji wa ndani wasiojitambua, wasiojituma, wasiojua maana ya timing ni kuviumiza vilabu vinavyoshiriki mashindano, hivi vilabu vinataka matokeo, vinataka mafanikio na ili wayapate haya ni lazima watafute watu wenye kuelewa nini maana ya kazi. Brazil hawazuii wachezaji kwenda kwao ila kwasababu wabrazili wanaeleweka kwa soka lao ndo maana utakuta kila club Ulaya kote kuna wabrazili lukuki,na nyinyi tengenezeni utaratibu wa kuwa na wachezaji wanouzika na kuitwa nje kulikoni mnaandaa mazingira ya kuzuia mapro eti ndo njia ya kukuza soka letu. Mkiwekeza kwenye academs ni dhairi mtapata wachezaji wanaofaa soko la ndani na muda si mrefu majirani zetu watakuja kununua vifaa kutoka Tz.
 
Back
Top Bottom