Tetesi: Uchaguzi Bodi Ya Ligi Ya TFF, KARIA, KIDAU na KUULI Kwenye Kashfa

Trump2

JF-Expert Member
Joined
May 28, 2017
Posts
1,553
Reaction score
2,609
Kesho tarehe 15/10/2017 ni siku ya Uchaguzi wa Bodi ya Ligi ya Shirikisho la Mpira sa Miguu Tanzania (TFF). Katika hali ambayo imewashtua wadau wengi wa Mpira wa Miguu, Rais wa TFF, bwana WALLACE KARIA akishirikiana na Kaimu Katibu Mkuu wa TFF, Bwana WIFRED KIDAU na Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF Bwana REVOCATUS KUULI kwa lengo la kutaka kumuweka mtu atakayelinda Maslahi yao na ambaye hatakemea vitendo vya rushwa ndani ya TFF , leo 14/10/2017 saa tisa mchana wanakutana kufanya kikao cha siri ili kumuwekea Zengwe mmoja wa wagombea nafasi hiyo ya Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi, Bwana CLEMENT SANGA, Kwa mujibu wa mhabarishaji ambaye ni mmoja wa Kamati Tendaji ya TFF ambaye hata hivyo hakufurahishwa na mpango huo, Mwenyekiti wa sasa wa Bodi hiyo anayemaliza muda wake, Bwana YAHAYA MOHAMED ndiye chaguo la Rais Bwana KARIA na mwenzake WILFRED KIDAU , chaguo ambalo hapana shaka siyo chaguo ya Wajumbe wote wa Mkutano wa kesho ambao kimsingi ndiyo wenye kuamua nani anafaa kuongoza Bodi ya Ligi siyo kwa maslahi ya watu wachache ndani ya TFF, bali kwa maendeleo ya Soka nchini
Itakumbukwa kwamba, kipindi hiki ambacho uongozi uliopo unamaliza muda wake, uongozi unaoongozwa na Mgombea anayepigiwa chapuo na Rais wa TFF, moja ya mambo ya hovyo kabisa tulioshuhudia ni Upangaji wa Ratiba ya Ligi uliochagizwa na rushwa na kujuana.

Mytake: Mamlaka husika zifanyie kazi Tuhuma hizi haraka sana kabla ya kesho

Mtonyaji.
 
Hao wote ni Simba. Wanahaha kuweka Simba mwingine pale.
Huyo Msomali ajiangalie sana. Atajikuta Mogadishu siku asiyotarajia.
 
Hao wote ni Simba. Wanahaha kuweka Simba mwingine pale.
Huyo Msomali ajiangalie sana. Atajikuta Mogadishu siku asiyotarajia.
Acha wakae Simba tupu nyie zamu yenu ilishapita
 
Kama ni kweli basi mwenyekiti mpya wa TFF anaanza vibaya. Mheshimiwa Malinzi alianza hivyo hivyo na mwishowe yamemkuta ya kumkuta. Yetu sisi ni macho na masikio tuu
 
Bongo hatuendelei MAJUNGU. Sasa mbona huyu uliyesema kawekewa zengwe kapita?!
 
Reactions: bdo
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…