Ni habari ambazo zimezagaa hapa mjini kuwa ma-super stars hawa wametosana!
Wenye taharifa kamili tunaomba data.
Siku nyingine ukitaka UDAKU nenda Globo, utashiba. Hizi habari zimeshapitwa na wakati!
Na Musa Mateja

Mastaa wa Kibongo waliowahi kuwa wapenzi na baadaye kutemana, Miss Tanzania 2006/07 anayefanya vyema kwenye tasnia ya filamu, Wema Abraham Sepetu na Charles Gabriel Mbwana Chalz Baba, wamerejesha rasmi mapenzi yao upya, Risasi Jumamosi linakuwa la kwanza kuibumburua.
TETESI ZAENEA, RISASI JUMAMOSI LAINGIA MZIGONI
Mei 7, mwaka huu, rafiki wa karibu wa Chalz Baba alilingata sikio gazeti hili kuwa, kuna kitu kinaendelea kati ya wawili hao.

Chanzo hicho kilidai kuwa, Chalz Baba amekuwa akipokea meseji kwenye simu yake kutoka kwa Wema akiomba warudiane.
Ukiachilia mbali meseji, kuna siku Wema alimpigia simu Chalz Baba nikapokea, akadhani anaongea na jamaa, akaanza kumuomba warudiane, kilimalizia chanzo hicho na kukabidhi majukumu kwa Risasi Jumamosi.
Gazeti hili lilizama mzigoni ambapo Mei 11, mwaka huu saa 9:00 usiku, Chalz Baba alinaswa akiwa na mrembo huyo nje ya nyumba ya akina Wema maeneo ya Sinza-Mori, Dar es Salaam.
Bila kuwashtua shushushu wetu aliwafuatilia hatua kwa hatua ambapo walionekana wakiwa wameweka mapozi mazito ya kimahaba huku wakijadili jambo fulani na kulumbana kiaina.
WEMA AMPA CHALZ BABA WARAKA WA MAPENZI
Katika harakati za kuachana kwa lengo la kwenda kumbonji, Wema alimuita Chalz Baba na kumtaka amgeukie.
Jamaa alipotii alichoombwa, Wema alionekana akimkabidhi zawadi ya kitambaa kilichopambwa na waraka wa maandishi ya kimapenzi ambayo Chalz Baba alisika akiyasoma kwa sauti na kuyafurahia kabla ya kukumbatiana na kudendeka kishkaji.
Risasi Jumamosi lilimtafuta Chalz Baba ili kuthibitisha kama kweli amerudiana na Wema ambapo bila hiyana, alifunguka:
Siwezi kusema tumerudiana lakini ni kweli tumekuwa na mawasiliano ya karibu sana kwenye simu na kukutana naye mitaani kama marafiki wa kawaida.
Unajua huwezi kuachana na mwanamke halafu mkashindwa hata kuwasiliana.
Paparazi wetu alipomtaiti juu ya kuwepo kwa ushahidi wa mawasiliano yao ya kimapenzi, Chalz Baba alitambaa na mistari:
Ni kweli katika siku za hivi karibuni Wema amekuwa akiniomba sana tuonane kwa ajili ya mazungumzo.
Siku hiyo baada ya kutoa burudani pale Billz (Bilicanas) nilimfuata Wema nyumbani kwao (Sinza-Mori) kwa kuwa aliniomba sana na sikuwa na ugomvi naye.
Tulizungumza fresh na baadaye kila mtu akaenda kulala kivyake.
Siwezi kukutamkia kwamba sisi ni wapenzi coz hatukukubaliana chochote kilichohusu uhusiano wetu wa kimapenzi.
Juhudi za kumpata Wema ziligonga mwamba lakini zinaendelea, akipatikana atafunguka laivu juu ya ishu hiyo na tutawaletea ripoti kamili.