Tetesi za soka Ulaya Ijumaa 06.08.2021: Messi, Kane, Lukaku, Correa, Trippier, Aouar, Abraham, Armstrong

Tetesi za soka Ulaya Ijumaa 06.08.2021: Messi, Kane, Lukaku, Correa, Trippier, Aouar, Abraham, Armstrong

Shujaa Mwendazake

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2015
Posts
4,016
Reaction score
6,759
Tangazo la Barcelona kwamba mshambuliaji wa Argentina Lionel Messi, 34, hatabakia kwenye klabu hiyo ''limefungua mlango wa uhamisho wa kushtua " katika Manchester City. (Manchester Evening News).

Uwepo wa Messi unaweza kuathiri uwezekano wowote wa uhamisho ambao Man City walikuwa wanaupanga kwa ajili ya mshambuliaji wa Tottenham na England Harry Kane, 27. (Express).

Paris St-Germain wamekuwa wakihusishwa moja kwa moja na Messi, lakini jiji kuu la Ufaransa linaonekana tu kama moja ya maeneo ambayo anaweza kwenda Muargentina huyo anayesakwa na klabu nyingi . (Le Parisien - in French)

PSG wanaonekana kuwa ndio wanaopendelewa kusaini mkataba na mshindi mara sita wa Ballon d'Or kuhamia, na uwezekano wake wa kuhamia Marekani kuchezea mojawapo ya Ligi Kuu pia upo . (Mail).

Romelu Lukaku

Chanzo cha picha, Getty Images
Pendekezo la Romelu Lukaku la kuhamia tena Chelsea huenda likawa linakaribia kukwama kwani mwenyekili wa klabu ya Milan Steven Zhang anataka kufikiria kwa muda zaidi kabla ya kuamua iwapo anataka kumuuza mshambuliaji huyo Mbelgiji mwenye umri wa miaka 28. (Gazzetta dello Sport - in Italian).

Manchester United bado wako makini na kusaini mkataba na mlinzi wa England Kieran Trippier, lakini Atletico Madrid wanakataa kupunguza bei yao ya pauni milioni 34 ili kumtoa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30. (Sun).

Arsenal wamefanya dau la takriban dola milioni 17 kwa ajili ya mshambuliaji wa klabu ya Lazio Muargentina Joaquin Correa, 26, ambalo "linaangaliwa kuwa halitoshi" na klabu hiyo ya Roma. (Corriere dello Sport, via Sport Witness).

Corea


Southampton wameuliza kuhusu taarifa za kusaini mkataba na Tammy Abraham, 23, kutoka klabu ya Chelsea kwa mkopo huku wakianza msako wao wa kumtafuta mtu atakayechukua nafasi ya mshambuliaji mwenzake wa England Danny Ings, 29, ambaye alijiunga na Aston Villa mapema wiki hii. (Talksport).

Arsenal wanapanga kusaini mkataba na mlinda lango wa England Aaron Ramsdale na kiungo wa kati wa Norway Sander Berge kutoka klabu ya Sheffield United, lakini dau la jumla la pauni milioni 50 huenda lisitoshe katika kuwapata vijana hao wawili wenye umri wa miaka 23 kila mmoja. (Star).

Mchezaji wa safu ya kati wa klabu ya Lyon Mfaransa Houssem Aouar, 23, amesubiri kuhamia katika klabu ya Arsenal msimu huu.(Sun)
Leicester wamejitokeza katika juhudi za kumuwinda kiungo mpya wa safu ya kati- ya mlinzi wa Ufaransa wa kikosi cha vijana wenye chini ya umri wa miaka 21 Wesley Fofana, 20, kupata jeraha la mguu wakati wa mechi ya kirafiki dhidi ya Villarreal Jumatano . (Sky Sports).

Mchezaji wa safu ya kati wa klabu ya Lyon Mfaransa Houssem Aouar

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,
Mchezaji wa safu ya kati wa klabu ya Lyon Mfaransa Houssem Aouar
Meneja wa Roma Jose Mourinho amaekuwa akihusishwa na taarifa za kumhamisha kiungo wa kati wa Cameroon kutoka Fulham mwenye umri wa miaka 25 Andre-Frank Zambo Anguissa, ambaye anaweza kuigarimu klabu hiyo ya Serie A takriban pauni milioni 21 . (Gazzetta dello Sport, via Sport Witness).

Brentford wanakamilisha kusaini mkataba na winga wa Congo winger Yoane Wissa mwenye umri wa miaka 24 , kutoka klabu ya Ufaransa ya Lorient. (Sky Sports).

Crystal Palace wako katika mazungumzo ya mwisho na Blackburn kuhusu mkataba kwa ajili ya mshambuliaji Muingereza Adam Armstrong mwenye umri wa miaka 24, ambaye thamani yake ni takriban pauni milioni 20. (Sky Sports).

Palace wanaongoza katika mbio za kupata sahihi ya Armstrong licha ya ofay a awali kukataliwa na Norwich City, Southampton na Watford zote wanaweka dau lao wenyewe. (Mail)
 
Back
Top Bottom