Jackson94
JF-Expert Member
- Sep 14, 2016
- 492
- 560
Chanzo cha picha,Getty Images
Everton wako tayari kumnunua winga wa AC Milan, Samuel Chukwueze, Manchester United wana matumaini ya kumsajili Alphonso Davies, Dusan Vlahovic bado anaweza kuhamia Arsenal.
Everton wanapanga kumsajili winga wa AC Milan kutoka Nigeria Samuel Chukwueze, 25, katika dirisha la uhamisho la mwezi Januari. (Football Insider)
Manchester United wanalenga kumshawishi beki wa pembeni wa Bayern Munich Alphonso Davies, 23, kuwachagua badala ya Real Madrid mkataba wa mchezaji huyo wa kimataifa wa Kanada utakapomalizika mwishoni mwa msimu huu. (Fichajes - kwa Kihispania)
Arsenal wanaweza kumpata Mserbia Dusan Vlahovic mwenye umri wa miaka 24, baada ya kumsaka kwa muda mrefu kwa bei nafuu kwa sababu mazungumzo ya mshambuliaji huyo wa Juventus na klabu yake kuhusu kandarasi mpya hayaendelei vizuri.(Caught Offside)
Unaweza Pia Kusoma
- Tetesi za Soka Ulaya Jumapili 20.10.202420 Oktoba 2024
- Tetesi za Soka Ulaya Jumamosi 19.10.202419 Oktoba 2024
- Mambo matano ya Ten Hag kuzingatia Man Utd12 Oktoba 2024
Chanzo cha picha,Getty Images
Meneja ajaye wa England Thomas Tuchel ametengana na mshirika wake wa muda mrefu wa ukufunzi Zsolt Low kabla ya kuchukua nafasi yake huko Three Lions. (Sun)
Aston Villa wameingia kwenye kinyang'anyiro cha kumsajili mshambuliaji wa Cameroon Bryan Mbeumo, 25, kutoka Brentford . (TBR Football)
Manchester United huenda huenda wakamuachilia kwa mkopo mshambuliaji wa Uholanzi Joshua Zirkzee, 23, kwa Juventus ikiwa watamsajili mshambuliaji wa RB Leipzig na Slovenia Benjamin Sesko, 21, msimu ujao. (Tuttomercato - kwa Kiitaliano)
Manchester City, Liverpool , na Tottenham wameelekeza macho yao kwa winga wa Real Valladolid Mhispania Raul Moro, 21. (Fichajes – kwa Kihispania)
Chanzo cha picha,Getty Images
Winga wa Borussia Dortmund Muingereza Jamie Bynoe-Gittens, 20, amezivutia Arsenal, Tottenham, Crystal Palace na Nottingham Forest - ingawa klabu hiyo ya Ujerumani inataka zaidi ya £50m kwa mchezaji huyo kabla ya kufikiria kumuuza. (Caught Offside)
Arsenal, Juventus, AC Milan na Napoli ni miongoni mwa vilabu vinavyomtazama kiungo wa kati wa Como na Argentina Nico Paz, 20. (Nicolo Schira on X)