Teuzi za Wakuu wa Wilaya: Je, wamefanyiwa vetting?

Chief Kabikula

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2019
Posts
7,567
Reaction score
9,037
Mkeka wa wakuu wa wilaya umetoka walioteuliwa wameonekana ambapo wengi ni watangazaji, wasanii, waigizaji na wengi ni vijana kweli.

Swali la msingi sio kuteuliwa bali ni je wamefanyiwa vetting kujua elimu yao, uwezo, tabia, mienendo, uzoefu, busara, hekima na makandondokando yao mengine na maana wengine tayari video zao za ufuska zimeanza kusambaa mitandaoni leo hii, sasa unajiuliza wamefanyiwa vetting kabla ya uteuzi? Au mradi liende?

Mama ana haki ya kuteua mtu yeyote yule lakini awe na sifa na uwezo wa kufanya kazi hiyo kitu ambacho kuna wengi hawana time will tell. Form Four failure kuwa mkuu wa wilaya kabisaaa?
 
Kama Katiba ya ccm ya mwaka 1977 inampa hayo mamlaka, sisi nani hata tumpinge? Siku ile Rasimu ya Katiba ya Jaji Warioba ikirejeshwa kwenye Bunge la Katiba, na yale mapendekezo yetu yakipitishwa kwa asilimia kubwa, nadhani haya madhaifu yote yataisha.

Ila kwa sasa ni haki yake! Hata akiamua kumteua mfanyakazi wake wa ndani, hakuna wa kumhoji.
 
Mkuu Chief Kabikula, ukuu wa wilaya hauhitaji elimu zaidi ya kujua kusoma, kuandika na kuongea.

U DED/U DAS na U RAS ndio shule inahitajika.

Vetting iliachwa tangu enzi za Mkapa. Vetting ya sasa ni "connection/kujuana/kuonekana na kujipendekeza".

Wateuliwa nao ni Watanzania, mchango wao unahitajika sana kuijenga Tz.

All in all, wakatimize majukumu yao kwa mujibu wa malelekezo ya nafasi zao na kwa mujibu wa sheria.
 
Mkeka wa wakuu wa wilaya umetoka walioteuliwa wameonekana ambapo wengi ni watangazaji, wasanii, waigizaji na wengi ni vijana kweli.

Swali la msingi sio kuteuliwa bali ni je wamefanyiwa vetting kujua elimu yao, uwezo, tabia, mienendo, uzoefu, busara, hekima na makandondokando yao mengine na maana wengine tayari video zao za ufuska zimeanza kusambaa mitandaoni leo hii, sasa unajiuliza wamefanyiwa vetting kabla ya uteuzi? Au mradi liende?

Mama ana haki ya kuteua mtu yeyote yule lakini awe na sifa na uwezo wa kufanya kazi hiyo kitu ambacho kuna wengi hawana time will tell. Form Four failure kuwa mkuu wa wilaya kabisaaa?
Vipi Mama amekusahau?
 
Duh!. Huu uteuzi wa ma-Dc mbona unahojiwa sana?. Au kuna watu walikuwa wanamatumaini ya kuteuliwa mkeka ukachanika?.

Nikki wa pili aliwahi kuimba sitaki kazi cha ajabu yeye kapewa kazi, huku vijana wengi wanaotafuta kazi hawazipati.
 
Mkeka wa wakuu wa wilaya umetoka walioteuliwa wameonekana ambapo wengi ni watangazaji, wasanii, waigizaji na wengi ni vijana kweli.

Swali la msingi sio kuteuliwa bali ni je wamefanyiwa vetting kujua elimu yao, uwezo, tabia, mienendo, uzoefu, busara, hekima na makandondokando yao mengine na maana wengine tayari video zao za ufuska zimeanza kusambaa mitandaoni leo hii, sasa unajiuliza wamefanyiwa vetting kabla ya uteuzi? Au mradi liende?

Mama ana haki ya kuteua mtu yeyote yule lakini awe na sifa na uwezo wa kufanya kazi hiyo kitu ambacho kuna wengi hawana time will tell. Form Four failure kuwa mkuu wa wilaya kabisaaa?
Hakuna vetting process, Msando asingekuwa DC, wengi tu hawana sifa ya kukamata nafasi Ile kuu ya wilaya. But anyway aliyepata ndio keshapata.

Bahati hiyo hata mie ningeipata ningeitumia vizuri japo nikitoka hapo niwe Nina mashamba, lodge zangu kadhaa, malori kadhaa ya transportation, biashara ya bima, hospital ya mama na watoto, na vimiradi vingine.
 
Back
Top Bottom