Daniel Mjema
Member
- Jul 23, 2007
- 77
- 84
Wana JF,
Salaam,
Nimelazimika kuileta makala hii ambayo ilichapishwa ukurasa wa 10 wa Gazeti la Mwananchi la Septemba 5 baada ya kupokea simu na meseji nyingi zikiniuliza ni aina gani ya Dawa ya Meno niliyokuwa naizungumzia katika makala yangu iliyokuwa na kichwa cha habari "TFDA ichunguze ukweli kuhusu dawa hii". Nimegundua kulikuwa na kosa la ufundi katika uhariri wa makala hiyo ambapo jina la Dawa liliondolewa na hivyo kupoteza mantiki nzima ya kutaka jamii ipate ujumbe huo. Kwa kutambua umuhimu wa makala hiyo, ndio maana nalazimika kuwaletea Original Version ya makala hiyo kama nilivyoituma kabla ya kuhaririwa.
Naomba radhi wale wote waliopata usumbufu huo.
TFDA ichunguze ukweli kuhusu dawa hii
Daniel Mjema
Dunia hivi sasa inatikiswa na taarifa za kisayansi kwamba dawa ya meno aina ya Colgate Total ina kemikali aina ya triclosan ambayo ina sababisha madhara ya ugonjwa wa Saratani ambao kisayansi hadi hivi sasa hauna tiba.
Taarifa hizi ni za kushtukia na kuogofya kwa vile dawa hiyo ya meno ipo katika maduka ya reja reja na maduka makubwa (Super Markets) hapa nchini. Kwa maneno mengine watanzania nao wako hatarini na tishio hili jipya.
Ni ukweli kuwa zipo aina ya Colgate ambazo zikiwamo zile zinazozalishwa kwa kutumia miti shamba. Hizi sio mlengwa wa makala hii ambayo naamini inasimama katikati kati ya maslahi ya umma na maslahi ya kibiashara.
Lakini pamoja na kuwapo kwa taarifa hizo, Tanzania ambayo inaaminika ni jalala la bidhaa kutoka nje haijachukua hatua madhubuti na makini kuhakikisha inawanusuru watanzania na matumizi ya dawa hiyo ya meno.
Nasema haijachukua hatua madhubuti na makini kwa sababu tangu kubainika kwa taarifa hizo, aina hiyo ya dawa ya meno imeendelea kuuzwa madukani bila hata kuthibitishwa kitaalamu (kimaabara) kwamba haina madhara.
Taarifa za kemikali hiyo aina ya triclosan inayohusishwa na ukuaji wa seli za Saratani, zimechapishwa kwa kirefu wiki iliyopita na vyombo vya kitaifa na kimataifa likiwamo gazeti dada la Mwananchi la The Citizen la Agosti 14.
Kwa faida ya wasomaji wa makala hii, mwaka 1997 Mamlaka ya Chakula na Dawa ya Marekani (FDA) mwaka 1997 iliruhusu matumizi ya dawa hiyo lakini chemikali zilizotumika zikafanywa siri hadi mwanzoni mwa mwaka huu.
Lakini kutokana na sheria ya uhuru wa vyombo vya habari, Shirika la Habari la Blomberg lilifungua kesi likitaka kemikali zilizotumika kuzalisha dawa hiyo ya meno ziwekwe wazi ili Jamii ijue mchanganyiko wake.
Wanasayansi watatu waliopitia ripoti ya FDA iliyowekwa kwenye mitandao ikiwa ni miaka 17 kupita tangu ianze kutumika duniani walibaini kuwa wazalishaji wa dawa hiyo hawakusema kila kitu (black and white) juu yadawa hiyo.
Taarifa zinasema wakati FDA ikiidhinisha dawa hiyo, iliegemea kwenye taarifa za kitafiti za wazalishaji wa dawa hiyo badala ya kuwajibika kikamilifu kuifanyia uchunguzi wa kimaabara na kujiridhisha kuwa ni salama.
Leo dunia nzima imetaharuki kwa vile dawa hiyo ndiyo inayoongozwa kwa mauzo katika nchi mbalimbali duniani ikiwamo Tanzania. Tunapaswa kujiuliza, kama kweli inaleta Saratani, ni watanzania wangapi wameshaathirika?.
Kemikali hiyo ya triclosan inaelezwa kupatikana pia katika baadhi ya sabuni na vipodozi na pia dawa za kuosha kinywa. Taarifa hizi si za kupewa uzito mdogo kama ilivyochukuliwa na mamlaka za hapa Tanzania.
Nimesoma kauli ya msemaji wa Mamlaka ya Chakula na Dawa Nchini (TFDA), Gaudensia Simwanza alipohojiwa na The Citizen akikiri kuwa wamepata taarifa zinazodai dawa hiyo ya Colgate Total ina kemikali hiyo yenye madhara.
Simwanza anasema tayari TFDA imeshawaagiza wataalamu wake kuifanyia kazi ripoti hiyo ili kujua hatima ya bidhaa hiyo kwenye soko la Tanzania na kwamba kwa ile iliyoidhinishwa hapa nchini ina asilimia 0.3 ya kemikali hiyo.
Kwa maelezo ya Simwanza, kiwango hicho hakina madhara kwa watumiaji wenye umri wa kati ya miaka 12 na kuendelea lakini swali la kujiuliza, ni je ni watanzania wangapi wanajua inapaswa kutumiwa na wenye umri huo?.
Wanasayansi wa Colgate wanawatoa hofu watumiaji wa dawa hiyo ya meno wasihofu kwani hatari ipo tu pale mtu atakapotumia kemikali hiyo kwa wingi. Swali la kujiuliza ni wingi upi unaozungumziwa hapa?.
Tangu mwanzo nilitangulia kusema kuwa nionavyo mimi, mamlaka zetu hazijachukua hatua madhubuti kukabiliana na hali hii kwa sababu ningekuwa mimi ndio TFDA, ningesimamisha kwa muda matumizi ya dawa hiyo.
Tutapoteza nini kama tutaisimamisha kwa muda wakati wataalamu wa TFDA wakifanyia kazi taarifa hizo kama ambavyo Simwanza anataka watanzania waamini?. TFDA inapaswa kujua kinga ni bora zaidi kuliko tiba?.
Sote tunafahamu namna Tanzania ilivyo jalala la bidhaa feki na za kugushi, TFDA ilipaswa iende mbali zaidi badala ya kuagiza tu wataalamu wake, wajue atakayepata Saratani watapaswa kujibu mbele za Mungu.
Watapaswa kujibu mbele za Mungu kwa sababu tumewakabidhi mamlaka zote za kushughulika na bidhaa za ina hii. Kama waliweza kuzuia matumizi ya maziwa ya watoto, kwanini wasizuie dawa hiyo kwa muda tukisubiri uchunguzi?.
TFDA ijue kuwa maisha ya watanzania yako mikononi mwao na ndio maana tangu mwanzo nilisema taarifa hii ya Colgate Total inashtua kama si kuogofya kwani imekuja wakati wagonjwa wa Saratani wakiongezeka nchini.
Ni bora tukajiridhisha kwanza juu ya taarifa hizi vinginevyo tujue majuto ni mjukuu!