Nduka
JF-Expert Member
- Dec 3, 2008
- 8,553
- 2,380
Hivi karibuni kumekuwa na taarifa za kufutwa kwa matumizi ya dawa za kikohozi na mafua kwa watoto chini ya miaka 12 na mamlaka nchini Kenya. Hali hii imetokana na madhara yanayosababishwa na dawa hizi. Kwa mujibu wa gazeti la Sunday News la tarehe 15 March 2009 tarifa za dawa hizi kuwa na madhara kwa watoto zipo tangu Julai mwaka 2007 ambapo kituo cha kuzuia na kudhibiti magonjwa cha Marekani(CDC) kilionya juu ya matumizi ya dawa hizi kufuatia vifo vya watoto watatu. Uchunguzi wa kituo hiki ulibaini zaidi ya watoto wengine 1,500 walifikishwa hospitali kwa matibabu ya dharura kutoka na matumizi ya dawa hizi. CHA KUSHANGAZA hapa Tanzania watendaji wa mamlaka ya udhibiti wa dawa na chakula wanadai wanaendele kuchunguza madhara ya dawa hizi.JE WANASUBIRI WATOTO WANGAPI WAFE ILI UCHUNGUZI WAO UWE UMEKAMILIKA?