Wakati mwingine sisi wengine tunashindwa kuelewa hiki kipengele cha mfungaji bora huwa kina maana gani, Je tunatafuta mfungaji/wafungaji bora au tunatafuta mtu mmoja wa kumpa zawadi?.
Kwa uelewa wa kawaida ukisema huyu ni mfungaji bora ina ndiye mwenye magoli mengi zaidi ya wenzake katika nyanja husika haijalishi hayo magoli yalipatikanaje aidha kwa kufungwa kwa kuotea,penati, mkono, makalio n.k.
Kama tunatafuta mfungaji bora basi haina maana ya kutafuta au kuweka kanuni nyingine zaidi ya mtu/watu wenye magoli mengi zaidi ya wengine kwani huyo ndiye au hao ndio wafungaji bora kwa sababu wana magoli mengi.
Tukianza kuweka kanuni za kuangalia nani ana assists nyingi au nani ana magoli machache ya penati baada ya watu kuwa na idadi sawa ya magoli basi lengo kuu litakuwa si kupata mfungaji bora bali ni kupata mtu mmoja wa kumpa zawadi.
Tukizingatia assists kuamua mfungaji bora tutakuwa hatutendi haki kwa sababu kuna nafasi nyingine katika soka ni ngumu sana kupata assist kwa kuwa hiyo nafasi anayocheza ndo inatakiwa kutumia hizo assist kutoka kwa wengine kufunga goli.
Tukizingatia magoli ya penati kuamua kumpata mfungaji bora napo tutakuwa hatutendi haki mana hata goli la penati nalo ni goli kama magoli mengine na kuna baadhi ya nyakati magoli ya penati ni magoli magumu zaidi kuliko ambayo hayajafungwa kwa penati, mfano katika mazingira ambayo goli la penati ndilo litaamua mshindi au hatma ya timu husika basi mpigaji wa penati atakuwa under pressure ambayo hii pressure hupelekea baadhi ya wachezaji/wapiga penati kutetemeka kwa woga au hata wachezaji wengine kukataa kupiga penati kutokana na pressure iliyopo. Lakini kuna magoli mengine ambayo hayajafungwa kwa penati ila ni magoli mepesi sana kuliko magoli ya penati.
Ushauri wangu kwa TFF au Bodi ya ligi hili swala la mfungaji bora lizingatie weledi na si mahaba. Tukisikia mfungaji bora basi imaanishe mtu/watu (m)wenye magoli mengi zaidi na si vinginevyo.