TFF au TPLB wataamua mfungaji bora kwa weledi au mahaba?

THE LINE

JF-Expert Member
Joined
May 19, 2023
Posts
202
Reaction score
308
Wakati mwingine sisi wengine tunashindwa kuelewa hiki kipengele cha mfungaji bora huwa kina maana gani, Je tunatafuta mfungaji/wafungaji bora au tunatafuta mtu mmoja wa kumpa zawadi?.

Kwa uelewa wa kawaida ukisema huyu ni mfungaji bora ina ndiye mwenye magoli mengi zaidi ya wenzake katika nyanja husika haijalishi hayo magoli yalipatikanaje aidha kwa kufungwa kwa kuotea,penati, mkono, makalio n.k.

Kama tunatafuta mfungaji bora basi haina maana ya kutafuta au kuweka kanuni nyingine zaidi ya mtu/watu wenye magoli mengi zaidi ya wengine kwani huyo ndiye au hao ndio wafungaji bora kwa sababu wana magoli mengi.

Tukianza kuweka kanuni za kuangalia nani ana assists nyingi au nani ana magoli machache ya penati baada ya watu kuwa na idadi sawa ya magoli basi lengo kuu litakuwa si kupata mfungaji bora bali ni kupata mtu mmoja wa kumpa zawadi.

Tukizingatia assists kuamua mfungaji bora tutakuwa hatutendi haki kwa sababu kuna nafasi nyingine katika soka ni ngumu sana kupata assist kwa kuwa hiyo nafasi anayocheza ndo inatakiwa kutumia hizo assist kutoka kwa wengine kufunga goli.

Tukizingatia magoli ya penati kuamua kumpata mfungaji bora napo tutakuwa hatutendi haki mana hata goli la penati nalo ni goli kama magoli mengine na kuna baadhi ya nyakati magoli ya penati ni magoli magumu zaidi kuliko ambayo hayajafungwa kwa penati, mfano katika mazingira ambayo goli la penati ndilo litaamua mshindi au hatma ya timu husika basi mpigaji wa penati atakuwa under pressure ambayo hii pressure hupelekea baadhi ya wachezaji/wapiga penati kutetemeka kwa woga au hata wachezaji wengine kukataa kupiga penati kutokana na pressure iliyopo. Lakini kuna magoli mengine ambayo hayajafungwa kwa penati ila ni magoli mepesi sana kuliko magoli ya penati.

Ushauri wangu kwa TFF au Bodi ya ligi hili swala la mfungaji bora lizingatie weledi na si mahaba. Tukisikia mfungaji bora basi imaanishe mtu/watu (m)wenye magoli mengi zaidi na si vinginevyo.
 
Wakati mwingine sisi wengine tunashindwa kuelewa hiki kipengele cha mfungaji bora huwa kina maana gani, Je tunatafuta mfungaji/wafungaji bora au tunatafuta mtu mmoja wa kumpa zawadi?...
Naomba ujitambulishe kwamba wewe ni Mchambuzi Bora kabisa hapa nchini. Kuanzia Sasa nitakufuatilia makala zako za JF na nje ya JF maana Una kitu.

Tunatafuta mfungaji Bora halafu tunauliza huyu kafunga Kwa ugoko yule kafunga Kwa kisigino?

Tunatafuta mfungaji Bora halafu tunajumuisha sifa za kiungo?
 
Wakati mwingine sisi wengine tunashindwa kuelewa hiki kipengele cha mfungaji bora huwa kina maana gani, Je tunatafuta mfungaji/wafungaji bora au tunatafuta mtu mmoja wa kumpa zawadi?...
Nina wasiwasi sana na hujuma zitazoweza kujitokeza, kwanini isitambulike sheria rasmi hata kabla ya Wafungaji magoli kulingana mwishoni mwa msimu wa ligi kuu?

Kuna kipi haswa kupelekea uwepo wa kikao cha bodi ya TFF?

Hakuna harufu za bahasha hapo?

Kwani ni hisani au juhudi binafsi za Mchezaji?

TFF huwa hawalijui hili miaka yote hadi pawepo na maamuzi yatayotokana na kikao bodi yao?

Africa hii daaaah [emoji848]

Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
 
Sheria za FIFA zipo kama Ifuatavyo.

1.Mchezaji akayefunga MAGOLi Mengi ndiye atakayepewa kiatu.

2.kama wachezaji watafungana tie kwenye MAGOLi Yao waliyofunga.
Aliyecheza michezo MICHACHE ndiye anakuwa amfungaji Bora.

3.kama wote wakilingana MICHEZO anapewa mchezaji MWENYE Asisist nyingi zaidi ya mwenzie.

Jf
 
Watumie Sheria za Fifa

Au wawape wote wawili
Ni kweli wapewe wote wawili kwa maana wamefanya kazi kubwa kila mtu kwa namna yake. Lengo ni kutambua juhudi zao katika ufungaji na si kushindanisha aina ya magoli yaliyofungwa wala nani alikuwa ana assist.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…