TFF badilisheni kanuni mwakilishi wetu kombe la Shirikisho CAF mwaka huu!

Jacobus

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2011
Posts
4,703
Reaction score
1,724
Ni dhahiri ratiba ya kombe la ligi ilikuwa ikipangwa kutegemea matokeo ya mechi ya timu za Azam, Simba na Yanga. Sasa timu hizo zimeotolewa katika michuano hiyo. Kwa utaratibu wa TFF mshindi ndo anayeiwakilisha nchi katika mashindano ya CAF yajulikanayo kama Shirikisho, mwaka huu timu moja wapo ya hizi "JKT Ruvu, Mtibwa, Singida United na Stand United " itaiwakilisha nchi yetu na hii itakuwa kinyume na matarajio ya TFF, hivo ni bora wakutane kwa dharura kuibadilisha ili mshindi wa pili kwenye VPL, inaweza kuwa Azam, Simba au Yanga, atuwakilishe msimu huu. Mshindi wa kombe la ligi apewe aksante tu.
 
Tumefungwa kizembe na possibly mwakani hatutawakilisha kombe lolote kwani......,
Yes, hii nayo inaweza kuwa sababu kwani timu pendwa tatu hazimo!
 
Subiri sindano ziwaingie vizuri. Maana mjue mwakani mtakuwa wa matopeni
 
Dawa imeingia vizuri.. Kuleni pilau lililopikiwa mafuta ya Alizeti kutoka Singida.
 
Matokeo yanabaki vile vile.Hii ni changamoto mpya ambayo itasaidia sana kukuza soka letu na hivyo kuchochea ushindani baina ya timu zetu.
 
Kwan hao wengine wanaoiwakilishaga nchi hufika wapi?
 
Yani ingewezeka hata ligi kuu wachukue wengine wakajaribu pia sio hawa mabwana SIMBA NA YANGA wanaenda kupoteza mda tu
 
Walipokuwa Yanga walifanya nini?? Afadhali waende JKT Ruvu kuliko Yanga.
 
Ukweli ningependa Singida watuwakilishe mwakani na wawe ndio wameingia kwenye ushindani wa kimataifa na taratiiiiiibu simba na yanga ziondoke kwenye utawala fake wa soka bongo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…