Mbabani
JF-Expert Member
- Jun 20, 2022
- 1,676
- 4,693
Salam wapenda "kandanda".
Kwa muda mrefu shirikisho la mpira wa miguu Tanzania limekuwa dhaifu inapotokea inshu ya SIMBA & YANGA. TFF na bodi ya ligi (bodi dhaifu kabisa) wanakua tayari kuvunja kanuni na sheria walizotunga wenyewe ili kuwanufaisha SIMBA & YANGA .
Hii derby ya 08/03/2025 Simba wamegomea na hawatafanywa kitu, Yanga waliwahi kugoma pia na hawakufanywa kitu.
Hii sio sawa kwa "afya ya soka la Tanzania". Watu walionunua tiketi kwa ajili ya mechi hii huenda wakawa wamepoteza pesa zao "kimasihara kabisa"
Kumekua na matukio ya upangaji matokeo na shirikisho lipo kimya (wao pia ni wahusika wa upangaji matokeo)
Viongozi wakubwa serikalini pia ni chanzo cha madudu haya katika soka letu.
Ni suala la muda tu ligi ya Tanzania bara itakuja kuporomoka vibaya sana.
Tunahitaji shirikisho na Bodi ya ligi imara ambayo "haitacheka na wowote" ili kuulinda mpira wa Tanzania.