ngulyavyangu
JF-Expert Member
- Jan 9, 2019
- 203
- 266
Mimi Kama mdau wa soka ninaumia Sana kuona mambo yanavyoendeshwa shaghalabaghala na Tff.
Tff Kama wasimamizi wakuu wa Mpira wetu, nadiriki kusema wameshindwa kuusimamia badala ya kutupereka mbele wao wanaturudisha nyuma.. Mfano mzuri Angalia ratiba ya ligi kuu utaelewa nini namaanisha.
Wakati ligi yetu inaendelea sisi wadau soka tulishangazwa kutoonekana viwanjani kwa kocha wetu mkuu wa timu ya taifa.
Tulitegemaea hauzulie hata baadhi ya mechi ili kuweza kuona ni mchezaji yupi anastahili kuitwa timu ya taifa.
Hiko kitu hakijafanyika, amunike alikua kwao Nigeria anakula mshahara tu, Yaani yeye ni kocha wa mechi tu, baada ya mechi huyoooo kwao Nigeria.
Sasa Nani alikua anafanya uchaguzi wa wachezaji Wakati yeye Hayupo?
Jibu ni kwamba kocha amefanya kwa mazoea.
Kwa mtazamo wangu kwakua kocha ni mgeni hawajui wachezaji wetu vizuri alipaswa kuwepo viwanjani ili kung'amua mchezaji yupi anastahili badala ya kutumia watu.. Hii ingesaidia hata Wakati wa upangaji kikosi, ila kwakua hawajui vizuri Hawa wachezaji mwisho wake ndio anatuwekea akina sonso full back Wakati huyu ni central back, kifupi huwa anabahatisha tu.
Tukiangalia kikosi kinamapungufu mengi Sana, Kuna baadhi ya wachezaji hawakustahili kuitwa na kunabaadhi ya wachezaji walistahili kuitwa ila wameachwa.
Hawa apa wachezaji walio stahili kuitwa ila hawajaitwa:
1)Paul Godfrey,
Kwanini alistahili?
Kwasababu baada ya kuuumia kwa kapombe kwa sasa Paul Godfrey ndie beki bora wa upande wa kulia kwa sasa.
Huyu dogo anakila kitu, nguvu, speed, driballing, uwezo wa kupiga Chenga uwezo wa kuzuia washambuliaji hatari, zaidi ni kasi yake inayo msaidia kurudi kwa Wakati eneo analo stahili kuwepo.
Kikubwa upande wa full back ya kulia kocha kamuita mchezaji mmoja tu, Hassan kessy, ivo akivurunda au akiumia Hakuna mbadala wake.
2)Hassan dirunga
Kwanini alistahili?
Ukiangalia performance yake kwenye ligi, Utaona ni mchezaji ambae alistahili kuwepo, dirunga anakupa vitu vingi kwa Wakati mmoja ambavyo vinakurahisishia kupata matokeo. Kwanza ni mbunifu, mnyumbufu, zaidi anauwezo Mkubwa wa kupiga Pass za mwisho,
3)ibrahim ajibu.
Kwanini alistahili?
Ajibu ni kipaji cha pekee Sana.
Ni marachache Sana kupata mchezaji Kama ajibu.
Ndio ajibu ni mwepesi, si mzuri kwenye kukaba, ila iyo aindoi ubora wake na kuona hastahili,
Tuna Timu ambayo IPO imara kwenye defence, Tuna timu ambayo inawashambuliaji hatari, ila tumekosa walishaji, ajibu alikua ndio solution wa ilo tatizo,
Ajibu anauwezo Mkubwa wa kupiga mipira iliyokufa, Ajibu anauwezo Mkubwa wa kupiga pass za mwisho, mwisho ni mfungaji mzuri.
Inaitaji roho mbaya kumuacha ajibu Kulingana na Aina ya kikosi ambacho kocha amekiita na Aina ya mechi labda tunatafuta sare.
4)Abdalah shaibu
Kwanini alistahili?
Ndie back bora wa Kati kwa sasa, ndio roho ya yanga kwa sasa, Dante na yondani wanapumzishana ila ninja hawamgusi kwa sasa,
Yondani amechoka kidogo Hayupo sawa, ninja ndie huwa ana clear makosa yake,
Ivoivo kwa Dante baada ya kutoka kwenye majeraha hajawa sawa, ninja ndie anaesawazisha makosa yake,
Ninja mipira ya juu ndio yake, anatumia nguvu na akili,
Mwisho kwenye tackling utampenda, anamahesabu mazuri Sana kwenye tackling.
5)mohamed Hussein "tshabalala"
Kwanini alistahili? Hakuna mwenye Maswali juu ya ubora wake, pia kocha kamuita left back mmoja tu so inashangaza kumuacha zimbwe junior.
Abdi banda
Kwanini alistahili?
Labda ana matatizo na kocha ila ni mchezaji ambae alipaswa awepo.
Hawa hapa wachezaji ambao hawakustahili
1)ulimwengu
Hajawai kuwa msaada kwenye timu.
2)mandawa Hana msaada kwenye timu
3)mudathil yahaya
Toka amerudi Azam hajarudisha kiwango kile alichokakionesha akiwa singida united.
Muda unashindwa kumuweka kwenye kundi gani, kiungo mkabaji au mshambuliaji, Yaani huwa anazurura tu Uwanjani na kupiga square pass mbili ya tatu kupoteza. Sio mzuri kwenye kukaba wala kushambulia,yupo slow Sana.
4)kennedy Wilson
Singida inapumulia mipira na kitasa wao ni huyu Kennedy, inaitaji bang ya arusha ili uweze kumuamini.
5)shiza kichuya.
Huyu kabaki jina tu,
Mwisho timu ya taifa inajengwa na wachezaji bora.
Timu ya taifa inaundwa na wachezaji walio na uzoefu wa mashindano makubwa, timu ya taifa Sio sehemu ya kuwafanyia majaribio wachezaji, mchezaji anaeitwa anatakiwa awe amekamilika.
Ivo ndivo wanavyofanya Wenzetu,
Sent using Jamii Forums mobile app