kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,778
- 14,214
Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo Na ukimzoea sana mbwa atakufuata hata msikitini.
Nimefurahi sana kuona timu zinazoshiriki michuano ya caf hazina vipolo kwenye ligi. Ila waamuzi wetu bado hawako kimataifa zaidi Bali wako kinjaanjaa Na kishabiki zaidi kwenye maamuzi Yao. Hali hii inawalemaza wachezaji na timu zetu kwenye mashindano ya kimataifa. Timu inayoonewa sana na waamuzi wetu ni rahisi sana kufanya vizuri kwenye mechi za kimataifa kuliko zile timu zinazodekezwa na waamuzi kwenye ligi.
Kuna wachezaji wanaocheza rafu mbaya kwa wenzao lakini hawaonywi inavyostahili na Kuna timu zinapewa advantage ya kufunga magoli kuliko timu nyingine. Yote haya yanalemaza wachezaji na timu Kimataifa na kuzighalimu timu kwenye mashindano ya kimataifa ambazo zinachezeshwa kimataifa zaidi.
Unapoona ligi yetu haitoi waamuzi kwenye mashindano ya kimataifa sio kwa bahati mbaya TU, bali tunafuatiliwa kimataifa pia, ni aibu kubwa kwa ligi yetu. Wachezaji wetu wanapewa kadi nyingi kwenye mechi za kimataifa, wanaotea sana, na kuzighalimu timu zao na hatimaye kupoteza mechi za kimataifa.
TFF kuweni wakali sana na waamuzi wenu wasiochezesha ligi kimataifa.