TFF hali tete, yahaha kusaka mdhamini mpya Ligi Kuu

TFF hali tete, yahaha kusaka mdhamini mpya Ligi Kuu

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
RAIS wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), Walace Karia amesema wapo kwenye mazungumzo na kampuni mbalimbali kwa ajili ya udhamini wa Kombe la TFF. Akizungumza na Waandishi wa Habari, Karia amesema kombe hilo halina mdhamini mkuu na hata kuitwa kombe la Shirikisho Azam ni kutokana na kutokuwa na mdhamini mwingine.

“Kombe linaitwa Azam kwa sababu tulisaini nao mkataba wa kuonyesha matangazo kwahiyo hakuna mdhamini mwingine ndio maana,” amesema Karia na kuongeza; Akitokea mdhamini mkuu basi jina lake litakaa pale, halafu hata kuitwa hilo jina ambalo linaitwa sasa ni kukosea maana jina lake ni kombe la TFF.”

Karia amesema wapo kwenye mazungumzo na baadhi ya kampuni kwa ajili ya kudhamini kombe hilo na akipatikan basi mdhamini jina lake litasimama kwenye Kombe rasmi.
 
Kasongo kazi yake nini au bodi ya ligi kiujumla kwani sio kazi ya TFF kutafuta mdhamini wa ligi
 
Hali tete kivipi!? Mbona unajichanganya mwenyewe kwenye maelezo yako!?
 
Back
Top Bottom