TFF huwa mnakuwa wapi vitendo vya kihuni vinapotokea uwanjani!?

severinembena

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2018
Posts
2,435
Reaction score
2,402
Our Game is Fair play!
Nilistaajabu sana Jana nilipokuwa naangalia mchezo kati ya timu ya Mbao FC dhidi ya Simba SC. Wakati Wa mapumziko wachezaji wakiwa wanaingia kwenye vyumba vya kupumzikia washabiki Wa Simba wakaanza kuwarushia makopo ya maji na kuwamwagia maji wachezaji Wa Mbao. Nikajiuliza hivi Mbao FC wamekosa nini? Sikuona wakiwachokoza washabiki au kufanya vitendo vya kuudhi wakati Wa mchezo. Na hata ingekuwa hivyo je hatua za kuchukuliwa ni kwa washabiki kukusudia kuwapiga/kuwajeruhi wachezaji Wa timu pinzani!?

Hivi TFF haya wameshayazoea na kuyafanya ni sehemu ya mchezo Wa mpira Wa miguu Tanzania!! Na viongozi Wa Simba,Mbao n.k haya wanayachukulia kwa wepesi na kuyafanya ni sehemu ya mpira wetu!? Manake sijaona kiongozi Wa Mbao FC akilalamikia hilo,na wala kiongozi Wa simba akikemea hilo.

Na ninyi Azam TV sijui kama mlirusha hivyo vitendo,na kama hamkurusha mlikuwa wapi au mlikuwa mnaona aibu kusha? Au mlikuwa mmetua chini kamera zenu baada ya kuchoka kuzibeba kwa muda mrefu!? Kumbukeni ninyi ni msaada sana ktk kuburudisha na kufichua uovu uwanjani.

Wallace Karia na jopo lako nyie endeleeni kukalia viti huko Karume na kupuuzia, bila kufuatilia na kuchukua hatua. Subirini mchezaji au kiongozi Wa klabu aje atolewe ngeu au kuzima ground ndo tuanze kulaani hivyo vitendo.
 
Tatizo njaa ndio zinazowafanya kutochukua maamuzi...wanafikiri kuwafungia washabiki wa timu fulani itawakosesha mapato wakt ndio wanajenga nidhamu ya soka letu na kulifanya liwe na hadhi...Njaa mbaya sanaa.
 
Tatizo njaa ndio zinazowafanya kutochukua maamuzi...wanafikiri kuwafungia washabiki wa timu fulani itawakosesha mapato wakt ndio wanajenga nidhamu ya soka letu na kulifanya liwe na hadhi...Njaa mbaya sanaa.
Sahihi asee
 
Sio mkia Fc tena ni kibindankoi haahahahja wazee soka limeanza washinda....mashabiki wameanza mwaga maji kama manabii
 
Yaani mashabiki wa simba wanadhani team ikienda kambi uturuki, team ikirudi ishinde mechi zote!
Haji Manara alisema mashabiki Wa Simba hawajui mpira bali wamejazana tu kwenye magroup ya Whatsap wanalaumu na kujadili mambo ya mpira wasiyoyajua
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…