TFF iachane na adhabu za kishamba

TFF iachane na adhabu za kishamba

The Boss

JF-Expert Member
Joined
Aug 18, 2009
Posts
49,282
Reaction score
117,244
Wakati Jose Mournho anaenda EPL ilikuwa inajulikana sifa yake ya kuongea ovyo ..wakati Fulani walimpa jina la "the mouth"...Mourinho alikuwa anafanya "mind games".

Akiwashambulia marefa kabla ya mechi ili waogope kuzigusa timu zake wachezaji wake wakicheza faulo....walichofanya EPL ilikuwa kumpiga faini za hela mara Kwa mara.

Hadi alipoondoka EPL alikuwa "kanyooka" ilifikia wakati akiulizwa swali anajibu "sitaki kuwapa hela FA".......adhabu za kufungia watu mda mrefu ni adhabu za kishamba Sana na za kizamani na za kukomoana.

wapo watu Kama Haji Manara wanachotaka ni attention na kuongelewa kila mara ..hata uwape adhabu IPI watamtafutia loopholes na kukukera zaidi na matokeo yake TFf Kama taasisi itaanza kuchafuka kuonekana "Wana personal issues" na wahusika.

Dawa ni faini za hela na uwaache aendelee na kazi yake Kwa mujibu wa mkataba wake na muajiri wake...wewe ambae sie muajiri wake why ujaribu kumzuia mtu asifanye kazi yake...wote waliofungiwa wafunguliwe.

Wapewe adhabu za faini...na pesa ikatwe Kwa waajiri wao.... tuache ushamba WA kukomoana.
 
Umezungumza vitu viwili tofauti epl na nbc apo kila lig ina kanuni zake kwahyo utaadhibiwa vile kanuni znataka
 
Kwani manara hajafungiwa wakati simba vinyesi fc mjibu
 
Adhabu za Tff ni za kukomoana mbaya zaidi Adui wa mtu mmoja mnalazimishwa taasisi nzima iwe Adui yenu.

Ndiomaana uongozi wa juu wa Tff ukiondoka wanao ingia wanafagia wote waliobaki kwakua waliambukizwa kufanya kazi Kwa chuki.
 
Bado watasema kuwa taasisi inaendeshwa kwa pesa za adhabu
 
Yani mtu kafa ya kosa na unakiti kuwa lile ni kosa ila bado hukubaliani na adhabu kwasababu adhabu inamtengenisha huyo mtu na taaluma yake?

Kwamba Manara ni mkubwa sana na yuko juu ya sheria kiasi yeye akihukumiwa basi lawama ziende TFF kwasababu mtu huyo hagusiki?

Mlikuwa wapi kutoa suggesyltions zenu wakati watu wengine wanafungiwa vifungo ambavyo huyu mnayemtetea leo alikuwa mstari wa mbele kushangilia adhabu walizopewa wenzake?

Acheni unafki
 
Siungi mkono hoja, watu wana pesa za mchezo huko toka kwenye biashara zao wavunje sheria makusudi then waachwe tu eti kwa kulipishwa faini!

Walivyo na akili ndogo watatumia hicho kigezo cha kulipishwa faini wazidi kuharibu makusudi ili kutuonesha wana pesa za kuchezea. Ulaya ni Ulaya tu, kamwe usilinganishe na bongo.

Naunga mkono adhabu za TFF ziendelee kuwanyoosha malimbukeni washamba wasio na weledi wa kutimiza majukumu yao ya soka.
 
Haji Manara amejaliwa mdomo mchafu! Atawezaje kukaa kimya? Yaani umfungie kusema mtu kama Haji Manara kweli! Mzee wa kukera!!

Aendelee tu kuwanyoosha hao TFF, Msomali Karia, na mbumbumbu wenzake waliomfundisha kutukana watu hovyo, na kutapika tapika tu maneno machafu.
 
Haji Manara amejaliwa mdomo mchafu! Atawezaje kukaa kimya? Yaani umfungie kusema mtu kama Haji Manara kweli! Mzee wa kukera!!

Aendelee tu kuwanyoosha hao TFF, Msomali Karia, na mbumbumbu wenzake waliomfundisha kutukana watu hovyo, na kutapika tapika tu maneno machafu.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] poleeeeeeh sio kwa kichefu chefu hicho, vipi nikuleteee diapers utapike???
 
Hilo nalo neno...

Kama vile makosa ya barabarani, unapigwa faini ya pesa unaendelea na maisha yako kama kawaida...
 
Kwamba ukipanga matokeo upigwe faini kisha uendelee na mechi inayofuata

Hata kadi nyekundu ulipe fedha kisha mechi inayofuata ucheze.
 
Ukitaka kujua Tff malofa, walisha wahi kutunga kanuni ya Vipensi kwaajili ya Zahera alipokua kocha wa Yanga baada ya kuondoka, Matola ana vaa na kanuni zimekufa.
 
Back
Top Bottom