Zak Malang
JF-Expert Member
- Dec 30, 2008
- 5,404
- 239
Wanajamvi, tujadili hili:
Hivi TFF imejipanga vipi kukabiliana na uwezekano wa suala la kupanga matokea katika mechi mbili zihusuzo watani wa jadi -- Simba na Yanga leo? Nasema hivi kwani uko uwezekano mkubwa sana kupanga matokeo -- hasa kuzirubuni/kuzihonga timu pinzani -- yaani Majimaji na Toto Afrika ili zikubali kufungwa idadi kubwa ya magoli ili moja ya timu hizo -- yaani Simba au Yanga inyakuwe ubingwa mwaka huu. Nasema hivi iwapo timu zote mbili yaani Simba na Yanga zitashinda mechi zao za leo, kwani tofauti ni goal difference.
TFF ni lazima iwe makini sana hapo. Ingawa bila shaka mechi zote mbili zitachezwa wakati mmoja, lakini kuna mawasiliano ya simu yanayoweza kutoa mwenendo wa mechi katika viwanja hivyo.
Mimi nadhani TFF iangalie sana idadi ya magoli, yakiwa mengi, basi bila shaka kutakuwa kamchezi ka kupanga matokeo. Ningeshauri hilo likitokea, TFF isimtangaze bingwa hadi kwanza ifanye uchunguzi wa kina kuhusu matokeo ya kila uwanja.