TFF imempiga faini ya shilingi millioni 1 na kumfungia mechi 5 Mchezaji wa Kagera Sugar, Juma Nyoso

Kunguru Mjanja

JF-Expert Member
Joined
Aug 22, 2012
Posts
2,046
Reaction score
3,971
Juma Nyoso.jpg

Shirikisho la soka nchini Tanzania (TFF) kupitia Kamati yake ya Nidhamu imemshushia adhabu kali mchezaji wa Kagera Sugar, Juma Nyoso kwa kosa la kumpiga shabiki baada ya mechi kati ya timu yake na Simba SC.

Kamati hiyo ya TFF iliyokutana Jumamosi iliyopita Februari 10, 2018 imemfungia Nyoso mechi tano na kumpiga faini ya shilingi 1,000,000 (Milioni moja) baada ya kikao hicho kujiridhisha kuwa mchezaji huyo alimpiga shabiki huyo.

Nyoso alimpiga shabiki baada ya mchezo wa ligi kuu soka Tanzania Bara kati ya timu yake ya Kagera Sugar dhidi ya Klabu ya Simba kwenye uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba mkoani Kagera.
 
astaafu tu naye mara awachome madole, mara vipepsi mara mateke... kweli bongo nyoso.
 
Nyoko nyoko kweli!

Mchezaji wa Kisasa Mwenye Tabia za kizamani na za kishamba
 
Huyu kaka namjua mtata tangu anakua tulikaa wote songea street Ilala na yule Said Morad watoto walikua wanamuogopa hana masihara.
 
Hahahaa, labda watampa kidogo mkuu.

Ila hii point nzuri sana japo fidia kidogo.

Kwa kweli inabidi kumpa fidia kidogo aliepigwa....itakuwa haina maana kama kipigo ule wewe halafu pesa wapige wengine
 
Huyu kaka namjua mtata tangu anakua tulikaa wote songea street Ilala na yule Said Morad watoto walikua wanamuogopa hana masihara.
Aah ww shakujua utakuwa tu fulani una jina linaanza na We.....
Kumbe umepiga ndindo ilala....
Ahhhh aha.....
 
View attachment 695086

Shirikisho la soka nchini Tanzania (TFF) kupitia Kamati yake ya Nidhamu imemshushia adhabu kali mchezaji wa Kagera Sugar, Juma Nyoso kwa kosa la kumpiga shabiki baada ya mechi kati ya timu yake na Simba SC.

Kamati hiyo ya TFF iliyokutana Jumamosi iliyopita Februari 10, 2018 imemfungia Nyoso mechi tano na kumpiga faini ya shilingi 1,000,000 (Milioni moja) baada ya kikao hicho kujiridhisha kuwa mchezaji huyo alimpiga shabiki huyo.

Nyoso alimpiga shabiki baada ya mchezo wa ligi kuu soka Tanzania Bara kati ya timu yake ya Kagera Sugar dhidi ya Klabu ya Simba kwenye uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba mkoani Kagera.

Huyu wanampendelea tu, ilibidi wamfunge miaka hata 10, faini ya milioni 40, na kama yote ingeshindikana wamnyonge tu kwani si mchezaji kweli ni mtoto wa kihuni tu anayependa mpira.
 
Back
Top Bottom