TFF imetumia kifungu gani kuwaadhibu Mbeya City kwa kosa la ball boys kuchelewesha mipira uwanjani kwenye mchezo wa Mbeya City vs Yanga?

NALIA NGWENA

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2016
Posts
10,587
Reaction score
13,425
Klabu ya Mbeya City imetozwa faini ya Tsh laki tano (500,000) kwa kosa la watoto waokota mipira (ball boys) kuchelewa kwa makusudi kurejesha mipira kiwanjani kwenye mchezo wa sare ya 3-3 dhidi ya Yanga uwanja wa Sokoine.

Maoni yangu TFF ilibariki kwa mikono miwili ball boys kuchelewesha mipira na kurusha mipira miwili miwili uwanjani kwenye game ya Taifa stars na Niger.

Sasa inakuawaje leo Club inapigwa faini wakati kitaifa Tff ilisimamia Hilo swala na ikawa furaha mioyoni mwetu na kuwasifu ball boys kuwa wamecheza Kama Pele.

Kama ndiyo hivyo hata Taifa stars Ipigwe faini kwa kuratibu upuuzi wa kurusha mipira miwili miwili uwanjani uwanjani kuliko kuwaonea Mbeya City.

Nawasilisha hoja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…