TFF inapenda dezo kutoka kwa Simba na Yanga

TFF inapenda dezo kutoka kwa Simba na Yanga

The Genius

JF-Expert Member
Joined
May 29, 2018
Posts
822
Reaction score
2,095
Mechi imeingiza 410M then mwenyeji anapewa 100M na ushee? Karibu 240M zimepotelea kwenye makato. Yaani makato ni makubwa kuliko mtaji. Biashara kichaa!

Hata mchanganuo haueleweki. Uwanja 47M, gharama za mechi 22M, ticket 22M. What the difference? Kama uwanja na ticket vimelipwa hizo gharama nyingine za mchezo ni zipi nyie vishohia?

Hiki ki-TFF cha Karia ni cha hovyo zaidi kuwahi kutokea tangu ikiitwa FAT. Bora hata enzi za Ndolanga na "wapigaji" wenzie kuliko hili genge la sasa.

Mwaka juzi Karia aliulizwa mafanikio ya TFF akasema Simba kufika Robo Fainali Klabu Bingwa Afrika. Yani jibu la ki-tabularasa kabisa. Timu Ligi Kuu ziko ngapi? Kwanini ujipime kwa Simba pekee? Na so far TFF imefanya nini specific kwa Simba ambacho ni tofauti na vilabu vingine?

Bila shaka sasa hivi akiulizwa swali hilo atasema mafanikio ya TFF ni pamoja na Yanga kufika Robo Fainali Shirikisho. Wakati anajua hakuna chochote specific ambacho TFF imefanya kwa Yanga wala Simba.

Ni juhudi zao binafsi, uongozi, wachezaji na benchi na ufundi. TFF hawajachangia chochote zaidi ya kula pesa za viingilio, kumfungia Haji manara na kutoa adhabu za ki-imla kwa yeyote mwenye maoni tofauti na genge lao.

Kwa kifupi TFF ya Karia inadidimiza soka kuliko kuendeleza. Timu inapata 410M unapiga panga 240M, halafu ikifanya vizuri kimataifa unajikomba kwayo. Idiot!

Shaffih Dauda amepigania sana soka la mtaani kupitia Ndondo Cup. Alistahili Nishani ya Heshima, lakini anaishia kupigwa majungu na haohao wanaojifanya kuendeleza soka. Soka gani mnaendeleza wakati kila mdau mnampiga vita?

Tarehe 26 April 2021 Karia aliliambia gazeti la The Citizen kuwa FIFA imewapa TFF $5M sawa na Tsh. 11 Bilioni kwa maendeleo ya soka nchini. Jiulize wamefanyia nini? Wameshindwa kuweka hata digital screen pale kwa Mkapa. Wameweka board za mabati ambapo mchezaji akijigonga anapata tetenasi.

Azam hawana pesa za FIFA lakini uwanja wao wameweka digital screen. Wanalipana mishahara mikubwa lakini wameshindwa kufunga screen? Ukihoji unafungiwa kujihusisha na soka. Upuuzi!

Hii iwe chachu kwa vilabu vikubwa kama Simba na Yanga kujenga viwanja vyao. Huu upigaji umezidi. Kati ya TFF na andazi, nachagua andazi. Stupid (in President Samia's voice)!

FB_IMG_1681987892533.jpg
 
Toa credit kwa ulikochukua taarifa kama mwenzio alivyofanya. Au wewe ndiye Malisa mwenyewe?

 
Mwaka juzi Karia aliulizwa mafanikio ya TFF akasema Simba kufika robo fainali klabu bingwa Afrika. Yani jibu la ki-tabularasa kabisa. Timu ligi kuu ziko ngapi? Kwanini ujipime kwa Simba pekee?
Si ndio iliyokuwa inashiriki, ulitaka aitaje na Mbeya City wakati CAF inaruhusu washiriki kuanzia mmoja hadi wawili? Wewe ni mjinga
 
Kikubwa hapo Wananchi hatukuwa wenyeji kwa hiyo waliopunjwa ni makolo, no mara waa!!
 
Mechi imeingiza 410M then mwenyeji anapewa 100M na ushee? Karibu 240M zimepotelea kwenye makato. Yani makato ni makubwa kuliko mtaji. Biashara kichaa.!

Hata mchanganuo haueleweki. Uwanja 47M, gharama za mechi 22M, ticket 22M. What the difference? Kama uwanja na ticket vimelipwa hizo gharama nyingine za mchezo ni zipi nyie vishohia?

Hiki ki-TFF cha Karia ni cha hovyo zaidi kuwahi kutokea tangu ikiitwa FAT. Bora hata enzi za Ndolanga na "wapigaji" wenzie kuliko hili genge la sasa.

Mwaka juzi Karia aliulizwa mafanikio ya TFF akasema Simba kufika robo fainali klabu bingwa Afrika. Yani jibu la ki-tabularasa kabisa. Timu ligi kuu ziko ngapi? Kwanini ujipime kwa Simba pekee? Na so far TFF imefanya nini specific kwa Simba ambacho ni tofauti na vilabu vingine?

Bila shaka saivi akiulizwa swali hilo atasema mafanikio ya TFF ni pamoja na Yanga kufika robo fainali shirikisho. Wakati anajua hakuna chochote specific ambacho TFF imefanya kwa Yanga wala Simba. Ni juhudi zao binafsi, uongozi, wachezaji na benchi na ufundi. TFF hawajachangia chochote zaidi ya kula pesa za viingilio, kumfungia Haji manara na kutoa adhabu za ki-imla kwa yeyote mwenye maoni tofauti na genge lao.

Kwa kifupi TFF ya Karia inadidimiza soka kuliko kuendeleza. Timu inapata 410M unapiga panga 240M, halafu ikifanya vizuri kimataifa unajikomba kwayo. Idiot.!

Shaffih Dauda amepigania sana soka la mtaani kupitia Ndondo Cup. Alistahili Nishani ya heshima, lakini anaishia kupigwa majungu na haohao wanaojifanya kuendeleza soka. Soka gani mnaendeleza wakati kila mdau mnampiga vita?

Tar 26 April 2021 Karia aliliambia gazeti la The Citizen kuwa FIFA imewapa TFF $5M sawa na TZS 11 Bilioni kwa maendeleo ya soka nchini. Jiulize wamefanyia nini? Wameshindwa kuweka hata digital screen pale kwa Mkapa. Wameweka board za mabati ambapo mchezaji akijigonga anapata tetenasi. Azam hawana pesa za FIFA lakini uwanja wao wameweka digital screen. Wanalipana mishahara mikubwa lakini wameshindwa kufunga screen? Ukihoji unafungiwa kujihusisha na soka. Upuuzi!

Hii iwe chachu kwa vilabu vikubwa kama Simba na Yanga kujenga viwanja vyao. Huu upigaji umezidi. Kati ya TFF na andazi, nachagua andazi. Stupid (in SSH's voice).!

View attachment 2594015
Ushauri wa bure; hivyo vilabu viwili vikongwe nchini vijenge viwanja vyao!

Mbona haya malalamiko hatuyasikii kule Chamazi Stadium? Yaani Azam ya mwaka 2010, ina uwanja wake wa kisasa! Halafu Yanga ya 1935, na Simba ya mwaka 1936, mpaka kesho inategemea uwanja wa Serikali!

Mambo mengine ni ya kujitakia tu.
 
Sorry moods najaribu kuibua hojA mpya lkn moods mnaunganisha na hojA ya Simba kuwa na viwanja. Hazihusiani naomba Uzi ujitegemee. K

Je Ni halali Tff, bmt, fa, na bodi ya ligi na gharama za mchezo kupokea mgao wa viingilio Hadi jumla ya m 100 mechi ya Simba Yanga wakati wazamini wa ligi Kama NBC na Azam Media Huwapa hulipia ma bilioni kwenye mikataba ya mashindano?

Naomba tujadili Nina hojA hapa.

🤔🤔👇👇👇


Mfano Sasa timu inazunguka kutafuta washabiki wajae uwanjani. Mechi ya wydad. Timu inazunguka kuuza tiketi. Wanafanya promo Alafu wanaambulia fedha kiduchu.
Mnawaumiza Sana wanaojitoa kusaidia hizi timu. Ndio maana ukimiliki timu bongo labda uwe fisadi

Mfano mechi ya Simba Yanga juzi Tff tu imechukua mamilioni karibu 100 kwa migongo mingi Sana

Eti gharama za mechi wahusika tff m. 22.. Je marefa waliongezeka? Au malipo yao Ni tofauti na mechi ya ihefu na polisi Tanzania? Kama gharama hizi Tff haihusiki unapata fedha za wazamini wa ligi NBC na warusha matangazo Azam Media za za Nini?!! Tff inapokea ma bilion kutoka NBC na Azam Media iache kung'ang'ania mapato ya uwanja na vilabu. Je inapewa ngao wa Nini kwenye mechi. Je gharama hizo Ni Zipi?

Baadae Tff wakachukua m 18. Eti kuwapa fa. Kweli? Zanini Sana wakati gharama za mechi walishajilipa tayari.

Hawakuridhika wakachukua Tena m 25. Eti bodi ya ligi. Kama gharama ya mchezo imelipwa, fa wakalipwa. Sasa na Hawa bodi hayo mamilioni ya Nini Sasa. Wakati bodi ya ligi Ni Hao Hao Tff. Hii Ni malipo mengine kwa kitu kimoja.

Hawakuridhika wakachukua Tena Tff m 10 kweli acheni Basi.



Ebu tujiulize he BMT si chombo Cha serikali?. Kinapokea bajeti toka serikali kuu. Je na chenyewe Kupewa m 10 sioni fear kabisa au kuwatuliza wasihoji?




Serikali simamieni utumike utaratibu wa haki.

Hawa Tff siwaelewi hapa
 
#MsasaSports MCHEZO WA SIMBA NA YANGA UMEINGIZA TSH. MILIONI 410...

Taarifa kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF inaeleza kuwa

"Mchezo wa Ligi Kuu ya NBC uliowakutanisha Simba SC na Young Africans uliochezwa Juma- pili Aprili 16, 2023 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam umeingiza jumla ya sh. 410,645,000.

Katika mchezo huo jumla ya mashabiki 53,569 waliingia ambapo VIP A waliingia Watazamaji 340 kwa kiingilio cha sh. 30,000 na kupatikana jumla ya sh. 10,200,000, VIP B waliingia

Watazamaji 4,160 kwa kiingilio cha sh. 20,000 ikapatikana jumla ya sh. 83,200,000. VIP C waliingia watazamaji 2,004 kwa kiingilio cha sh. 15,000 na kupatikana sh. 30,060,000 wakati jukwaa la rangi ya Machungwa waliingia watazamaji 10,372 kwa kiingilio cha sh.

10,000 ikapatikana jumla ya sh. 103,720,000 na jukwaa la mzunguko waliingia Watazamaji

36,693 kwa kiingilio cha sh. 5,000 na kupatikana jumla ya sh. 183,465,000.

Mgawanyo wa mapato

VAT Sh. 62,640.762.71

BMT Sh. 10,440,127.12

Gharama za tiketi Sh. 22,585,475

Uwanja Sh. 47,246,795.28

Gharama za mchezo Sh. 22,048,504.46

TFF Sh. 12,599,145.41

TPLB Sh. 25,198,290.81

FA Mkoa Sh. 18,898,718.11

Timu mwenyeji (Simba SC) Sh. 188,987,181.10

#MsasaKisasaZaidi.
 
Ushauri wa bure; hivyo vilabu viwili vikongwe nchini vijenge viwanja vyao!

Mbona haya malalamiko hatuyasikii kule Chamazi Stadium? Yaani Azam ya mwaka 2010, ina uwanja wake wa kisasa! Halafu Yanga ya 1935, na Simba ya mwaka 1936, mpaka kesho inategemea uwanja wa Serikali!

Mambo mengine ni ya kujitakia tu.
Hata wakijenga viwanja kitakachookolewa ni kidogo kwa makato hayo
 
Nitakuwa mtu wa mwisho kuamini mechi Ile imeingiza 410M, naamini ni zaidi ya iliyosemwa
 
Hata wakijenga viwanja kitakachookolewa ni kidogo kwa makato hayo
Mimi naona wakijenga viwanja vyao, wataokoa kiasi kikubwa tu cha pesa. Makato makuu hapo yatakuwa ni ya kodi tu. Hizo takataka nyingine hapo juu, sidhani kama nazo zinastahili kupewa mgao kwenye viwanja binafsi.
 
Mimi naona wakijenga viwanja vyao, wataokoa kiasi kikubwa tu cha pesa. Makato makuu hapo yatakuwa ni ya kodi tu. Hizo takataka nyingine hapo juu, sidhani kama nazo zinastahili kupewa mgao kwenye viwanja binafsi.
Natamani sana kujua upande wa Azam fc hali ipoje kwa uwanja wao. Isijekuwa nao pamoja na kuwa na uwanja wao lakini BMT, TPLB, TFF, FA mkoa nao wanakatwa.
 
Huyo karia unamuonea tu, huo mgawanyo ulikuwa hivyo hivyo hata kabla Karia hajawa rais
 
Natamani sana kujua upande wa Azam fc hali ipoje kwa uwanja wao. Isijekuwa nao pamoja na kuwa na uwanja wao lakini BMT, TPLB, TFF, FA mkoa nao wanakatwa.
Siamini kama watakuwa wanasogeza pua zao kwenye viwanja binafsi.
 
Ushauri wa bure; hivyo vilabu viwili vikongwe nchini vijenge viwanja vyao!

Mbona haya malalamiko hatuyasikii kule Chamazi Stadium? Yaani Azam ya mwaka 2010, ina uwanja wake wa kisasa! Halafu Yanga ya 1935, na Simba ya mwaka 1936, mpaka kesho inategemea uwanja wa Serikali!

Mambo mengine ni ya kujitakia tu.
Jamani, Tanzania tunajuana. Hao viongozi wabadhilifu kwa kushirikiana na viongozi wa Simba na Yanga, hawawezi kuruhusu Simba na Yanga zikajenga viwanja vyao.

Hapa ni kama vile tunawatetea Simba kupata mgao mdogo, lakini unakuta viongozi binafsi wa Simba wamelambishwa asali ya kutosha, halafu wanabaki wanatucheka mashabiki
 
Back
Top Bottom