Binafsi nimeipokea kwa masikitiko makubwa taarifa hii ya TFF ya kupiga marufuku kuvaa mavazi ya vyama au yenye muelekeo wa vyama fulani, ningependa kujuzwa kuhusu timu yangu ambayo Jezi zake zina muelekeo wa moja kwa moja na Chama
fulani.
Tunawaomba TFF kipindi hiki cha kampeni watuache huru kwani ipo siku maalumu ambayo tumezuiwa kufanya hivyo nayo ni ile siku ya kupiga kura, vinginevyo siioni mantiki ya TFF kuzuia uvaaji wa nguo hizo katika kipindi hiki cha kampeni kwani itakuwa inakipendelea zaidi chama fulani kwa upande wa mavazi.