TFF inavyoiba mapato kwa kushirikishana na Serikali!!

TFF inavyoiba mapato kwa kushirikishana na Serikali!!

kipumbwi

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2015
Posts
3,162
Reaction score
9,073
Wadau naomba nijielekeze kwenye mada tajwa.

Wengi tunajua mechi za Simba na Yanga huwa ni tukio la kitaifa kama sio kimataifa na hugusa watu wengi,bahati mbaya naona Kuna kikundi kichache daima kinatumia mgongo wa Simba na Yanga kufanya wizi wa mapato.

Kuelewa hili kwanza tutazame taarifa rasmi ya TFF kuhusu mapato na migawanywa
IMG-20230420-WA0020.jpg

Sasa tutazame wizi ambao umefanyika hapo.
Wizi wa kwanza hapa umefanywa na serikali,wizi kwa kua serikali imechukua fedha mara 3
1. VAT 62,640,762
2. BMT 10,440,127
3. Uwanja 47,246,795
Jumla Tshs120,427,684 hizi za Serikali. Klabu hapo imegawana nusu ya mapato ya ilichopata na serikali.

Wizi wa pili,huu umefanywa na TFF kwa kuchukua fedha za klabu mara 4

1. TFF 12,599,145
2. Bodi 25,198,290
3. DRFA 18,898,718
4.G/Mchezo 22,048,504
Jumla Tshs78,744,657 hizi za TFF

Tickets ukinunua unalipa VAT, N-card ukinunua unalipia VAT,makusanyo yanakatwa VAT 18%

Kama kila shabiki alienunua tiketi amekatwa VAT,hizi gharama nyingine za VAT za nini?!! Sio double taxation?!! Sio wizi?!!

Simba na Yanga zinatumia gharama kubwa sana kuendesha timu,fedha zinaibwa kijanja na wahuni wachache.
 
Kuhusu Simba na Yanga endeleeni kupihwa Kwa sababu watanzania ni wajinga ,kila siku tunasema tunataka katiba mpya ambayo itadunga sindano kila eneo la nchi lakini vijana mpo busy kuwa machawa wa CCM ,hayo ni matokeo ya ubinafsi hivi mnawaza watoto wenu wataishi vipi kesho hapa Tanzania!yaani mumefanywa wajinga na ccm hadi mnafurahia umaskini aiseeee Acha tupigweeeeee
 
Nimetafakari sana, sijui kwa nini timu zenyewe ziko kimya. Ziandae Kambi, zilipe makocha, zilipe mishahara ya wachezaji inapokuja kwenye mapato, zinaambulia 46% pekee.
Sijui labda timu zinaelewa ndo maana ziko kimya. Hatariii
 
Hakuna walicho ibiwa maama Simba ,Yanga na serikali ni kitu kimoja.
 
Kwano hayo makato yanakuwepo pia katika viwanja binafsi vya timu? Mfano Chamazi Stadium, Majaliwa Stadium, nk?

Kama hakuna utitiri wa makato kama hayo; kwa nini hivi vilabu visijenge viwanja vyao, ili kuondokana na huu unyonyaji?

Yaani timu zimeanzishwa miaka ya 1930's, lakini mpaka leo bado vinaendeshwa kama taasisi za serikali!
 
Hakuna walicho ibiwa maama Simba ,Yanga na serikali ni kitu kimoja.
Simba na Yanga ni za wananchi kama Mimi nawewe, viongozi wao ndio hujikuta wanachotwa na watawala na kutumika kufanya propganda za kusifia watawala kama tunavyoonaga mabango na kauli za kisiasa za kusifia watawala,ilihali hata muongozo ya FIFA inapiga marufuku mechi kua na mambo yenye taswira ya kisiasa!!
 
Wadau naomba nijielekeze kwenye mada tajwa.

Wengi tunajua mechi za Simba na Yanga huwa ni tukio la kitaifa kama sio kimataifa na hugusa watu wengi,bahati mbaya naona Kuna kikundi kichache daima kinatumia mgongo wa Simba na Yanga kufanya wizi wa mapato.

Kuelewa hili kwanza tutazame taarifa rasmi ya TFF kuhusu mapato na migawanywaView attachment 2594382

Sasa tutazame wizi ambao umefanyika hapo.
Wizi wa kwanza hapa umefanywa na serikali,wizi kwa kua serikali imechukua fedha mara 3
1. VAT 62,640,762
2. BMT 10,440,127
3. Uwanja 47,246,795
Jumla Tshs120,427,684 hizi za Serikali. Klabu hapo imegawana nusu ya mapato ya ilichopata na serikali.

Wizi wa pili,huu umefanywa na TFF kwa kuchukua fedha za klabu mara 4

1. TFF 12,599,145
2. Bodi 25,198,290
3. DRFA 18,898,718
4.G/Mchezo 22,048,504
Jumla Tshs78,744,657 hizi za TFF

Tickets ukinunua unalipa VAT, N-card ukinunua unalipia VAT,makusanyo yanakatwa VAT 18%

Kama kila shabiki alienunua tiketi amekatwa VAT,hizi gharama nyingine za VAT za nini?!! Sio double taxation?!! Sio wizi?!!

Simba na Yanga zinatumia gharama kubwa sana kuendesha timu,fedha zinaibwa kijanja na wahuni wachache.
Umeandika hoja nzuri sana.
 
Back
Top Bottom