tatum
JF-Expert Member
- Jan 16, 2018
- 5,786
- 4,491
Toka Ligi Kuu ya Tanzania Bara imeanza msimu wa 2018/2019 kwa kujumuisha timu 20 kwa lengo la kuboresha Ligi lakini na kuongeza wigo wa timu nyingi kushiriki kumekuwa na tatizo kwenye kamati inayoshughulikia Ratiba ya Ligi kwa ujumla wake.
Kabla ya kupanga Ratiba ya Ligu Kuu ni matumaini yangu kuwa Kamati husika iliangalia mashindano mengine yote ambayo yapo mpaka michezo ya Timu ya Taifa.
Wakati wenzetu nchi mbalimbali katika ligi zao huwezi kuyakuta hayo lakini kwa Tanzania imekuwa kama desturi tu na hakuna anayeona kama ni tatizo.
Ukiangalia jinsi ambavyo timu zinapangiwa ratiba unaona kabisa hapo kuna tatizo kubwa sana.Yanga imecheza michezo 7 wakati baadhi ya timu zimecheza mzunguko wa 11 timu kama Singida UTD,Mbao FC,Coast Union,Alliance na Tanzania Prisons FC.Timu zingine zimecheza michezo 10 kama Azam wengine michezo 9 kama Simba na Mwadaui FC
Kwahiyo unakauta hata ukisikia fulani anaongoza Ligi lakini amecheza michezo mingi kuliko wengine na hao wengine wakichezo na kufikia michezo aliyochezo huyo anayeongoza ligi na wakashinda yote wanampita .
Kwahiyo unakuta haileti maana yoyote kuwa pale juu kuongoza ligi wakati wengine wamechezo michezo michache.Hilo huwezi kabisa kulikuta nchi zingine kama England,Spain,Ujeruman,Ufaransa,Kenya,South Africa,Nigeria n.k
TFF hilo mnalijua kabisa na mnapanga kwa makusudi kwanini nchi zingine waweze wakati hapa Tanzania tunashindwa kuhakikisha kila timu mwisho wa wiki wote wanakuwa na michezo sawa waliocheza? kama ni tofauti basi ni mchezo mmoja tu tena kwa timu moja au mbili tu.
Rais Magufuli amesema juzi hapa kuwa anataka mabadiliko kwenye michezo na anataka timu zifanye vizuri kwa kuwa na mipango mizuri ya kuendeleza michezo nchini kwa vyama vyote vya michezo sasa TFF kama hili dogo tu la ratiba linawashinda je hayo makubwa mtayaweza kweli kama Rais Magfuli anavyotarajiwa?